Posts

Showing posts from December, 2025

TUME KUTATHIMINI FIDIA MIRADI SMZ

Image
                                           Na Mwandishi Wetu, Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ameunda Tume ya  Watu nane kupitia na kutathmini masuala ya fidia kufuatia utekelezaji miradi  ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Unguja na Pemba. Taarifa kwa vyombo vya habari leo 31 Desembaa 2025 na kusainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Raqey Mohamed ilisema tume hiyo itakuwa na jukumu la kupitia masuala ya fidia na changamoto zilizojitokeza na kuishauri serikali kuchukua hatua stahiki. Taarifa hiyo imewataka wananchi kuipa ushirikiano tume hiyo pindi itakapofika maeneo husika kwa ajili ya kupata taarifa stahiki kuhusiana na kazi walizopangiwa. Tume inaundwa na wabobezi katika fani tofauti ambao ni pamoja na Salim Othman Simba ambaye ni mtumishi wa umma mstaafu na mtaalam wa Uthamini. Yupo pia  Mussa Kombo Mrish...

BALESI KOCHA MPYA KMC

Image
 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TIMU ya Soka ya KMC, imemtangaza Abdallah Mohamed Juma 'Balesi' kuwa kocha mkuu wa timu hiyo inayosua sua katika Ligi Kuu ya NBC. Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa uongozi wa timu hiyo kuachana na aliyekuwa kocha mkuu, Marcio Maximo. Akitangaza hatua hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, Meya Songoro Mnyonge  alisema wameamua kuachana na Maximo kutokana na mwenendo wa matokeo yasiyoridhisha. "Malengo na mkakati ya halmashauri ni kuwa na matokeo makubwa haikuweza kutimia sio kwamba kocha hakuwa mzuri ila alikuwa na malengo ya muda mrefu hivyo tukaamua kuachana nae" alisema Songoro. Mkurugenzi wa Manispaa Kinondoni, Hanifa Suleiman Hamza alisema kuwa Manispaa Kinondoni imeamua kufanya uwekezaji mkubwa hivyo inafanya maboresho yanayofanana na thamani ya uwekezaji ndio maana wakaamua   kubadili upepo kwa kumchukua kocha mwingine kuendeleza timu. Kocha Balesi alisema ana uzoefu wa majukumu ya aina  hiyo na sehemu zote ali...

Taifa Sars yafuzu 16 Bora

Image
 

CCM YASHINDA UCHAGUZI MDOGO FUONI

Image
                                            Na Mwandishi Wetu, Zanzibar CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimeshinda uchaguzi Mdogo Jimbo la Fuoni, Mkoa wa Mjini Magharibi katika matokeo yaliyotangazwa usiku wa 30 Desemba 2025. Msimamizi wa uchaguzi wa wilaya, Miraji Mwadini Haji alimtangaza mgombea wa CCM, Asha Hussein Saleh kuwa mshindi kwa kupata kura 9,861. Aliyemfuatia ni Khamis Shaibu Mussa aliyeambulia  kura  503 kati ya kura zote 11,024 zilizopigwa. Kulingana na msimamizi huyo, waliojiandikisha  ni 14,130 na kura 94 ziliharibika. " Kwa mantiki hiyo namtangaza Asha Hussein Saleh wa CCM kuwa ndie mshindi Jimbo la Fuoni" alisema msimamizi huyo.

WIZARA YA ELIMU YAUKANA WARAKA

Image
 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imekanusha taarifa zilizosambazwa mtandaoni kuwa shule hazitafunguliwa Januari na kueleza kuwa ratiba za mihula ya masomo ipo kama ilivvyopangwa. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo  cha Mawasiliano ya Serikali, Sylivia Lupembe ilisema shule za Awali, Msingi na Sekondari zitafunguliwa 13 Januari 2026. "Tunapenda kuufahamisha umma wa waTanzania na wadau wote wa elimu ratiba ya mihula imeshatolewa na wizara kupitia Waraka wa elimu namba 5 wa 2025 na Waraka namba 6 wa mwaka 2025 kuhusu mihula ya masomo zilizotolewa 19 Novemba 2025 kuzingatia kalenda hiyo" ilisema taarifa hiyo. Taarifa hiyo imewataka wananchi kulipuuza tangazo hilo na kuzingatia kalenda iliyotolewa awali na wizara.

DKT. MWINYI AONGOZA KIKAO BARAZA LA MAPINDUZI

Image
                                           Na Mwandishi Wetu, Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 29 Disemba 2025, ameongoza Kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi (BLM) katika kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Nane. Kikao hicho kimefanyika Ikulu, Zanzibar na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

MBETO: VYAMA VIHESHIMU KATIBA ZANZIBAR

Image
                                           Na Mwandishi Wetu, Zanzibar CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kinasema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa nafasi nyeti kwa uchumi wa Zanzibar kwa mawaziri wanne toka ACT Wazalendo ambao hata hivyo hadi sasa hawajashiriki kuunda Serikali ya Umoja wa kiTaifa   ( SUK ) kama Katiba ya Zanzibar inavyoelekeza. Kulinga na Katiba ya Zanzibar chama kinachofuatia kwa wingi wa kura katika Uchaguzi Mkuu, hutoa Makamu wa Kwanza wa Rais na hupewa nafasi  za maWaziri kulingana na wingi wa Viti vya Wawakilishi walivyoshinda ndani  ya siku tisini. Akizungumza katika ziara za Rais Dkt. Hussein Mwinyi ambazo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu Mkuu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema kutokana na unyeti wa ...
Image
 

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

Image
                                          Mwandishi Wetu, Zanzibar CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakitamvumilia mteule yeyote wa Rais wa Awamu ya Nane, Dkt. Hussein Ali Mwinyi wala taasisi yoyote itakayoshindwa kusimamia utunzaji wa miundombinu ya  kisasa  inayojengwa  Zanzibar kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Akitoa tathmini   ya ziara inayoendelea ya Rais Dkt. Mwinyi  ya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu wa  Kamati Maalum NEC, Zanzibar Idara  ya  Itikadi,Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis  alisema  kote walipoenda katika ziara hiyo, Rais Dkt. Hussein Mwinyi anasisitiza utunzaji miundombinu. "CCM tunaunga mkono kauli yake na tunafuatilia na tunasisitiza kuwa hatutamvumilia mteule  au mtendaji yeyote atakaye zembea kwenye eneo lake n...

DKT. MWINYI: TUTAENDELEA KUJENGA SHULE ZA GHOROFA

Image
 Na Mwandishi Wetu,, Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea na ujenzi wa shule za ghorofa kama suluhisho la kudumu la changamoto ya uhaba wa madarasa na kuondoa hali ya watoto kuingia madarasani kwa zamu, asubuhi na mchana. Ameeleza kuwa lengo la Serikali ni kuongeza bajeti ya sekta ya elimu hadi kufikia TSh.Trilioni Moja na kuifanya kuwa sekta mama ya kipaumbele kwa maendeleo ya nchi. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 27 Disemba 2025 alipoifungua Shule Mpya ya Msingi ya Kisasa ya Muungano iliyopo Kibanda Maiti, Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Amefahamisha kuwa katika utekelezaji wa mkakati huo, tayari Serikali imeshasaini mkataba na Benki ya CRDB wenye thamani ya Tsh. Bilioni 240 kwa ajili ya ujenzi wa shule 29 za ghorofa, na kwamba maandalizi ya ujenzi huo tayari yameanza katika maeneo ya Fuoni Kibondeni, Jumbi na Chunga kwa Unguja, ...

DKT. MWINYI: WEKEZENI KATIKA VITU VIKUBWA

Image
 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza watu wenye maeneo mazuri kufanya  vitu vikubwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa badala ya vidogo visivyo na tija ili wao wenyewe na serikali kunufaika na pia kuufanya mji kuwa na mandhari ya kupendeza kama walivyofanya  Umoja wa Walemavu Zanzibar. Wito huo ameutoa 23 Desemba 2025 mara baada ya uzinduzi wa nyumba za kisasa  katika 'Mji wa Dkt. Hussein Ali Mwinyi' ambao umeanzishwa, Mombasa, Mkoa wa Mjini, Unguja. Mradi huo ambao umekamilika ni wa majengo 14 yenye ghorofa 5 yakiwa na nyumba 276 za kisasa, umegharimu TshBilioni 34, chini ya Mfuko wa Hifadhi ya Wafanyakazi Zanzibar (ZSSF) na kujengwa na Kampuni ya CRJE ya China. Dkt. Mwinyi alisema wakati wa uzinduzi wa nyumba hizo kuwa anaupongeza umoja huo kwa uamuzi wao wa kukubali eneo hilo kujengwa mradi huo jambo ambalo litawanufaisha wao, serikali na wananchi. "Eneo hilo  wenye ulemavu wangeweza...

ACT WAITWA KUUNDA SERIKALI ZANZIBAR

Image
                                           Na Mwandishi Wetu, Zanzibar CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kina imani na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwani ndio mfumo ambao waZanzibari waliuchagua. Akizungumza Ofisini kwake, Kisiwandui Unguja. Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema njia ya kutatua changamoto za waZanzibari ni kufanyakazi pamoja. Kulingana na  Katiba ya Zanzibar, chama  kinachoshika nafasi ya pili kwa wingi wa kura hutoa Makamu wa Kwanza wa Rais na wingi wa viti vya Uwakilishi chama hicho hupata  nafasi za Uwaziri na mchakato huo unatakiwa ukamilishwe ndani ya siku tisini. Alisema kutokana na ACT Wazalendo kupata viti 10 vya Uwakilishi katika Uchaguzi Mkuu uliopita 29 Oktoba 2025, inapata nafasi 4 za uWaziri lakini hadi sasa vipo wazi wakati shughuli za serikali zinaendelea. "Ukis...

DKT. MWINYI; ZSSF WEKEZENI MIRADI YA UMEME

Image
 Mwandishi Wetu, Zanzibar RAIS wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi angependa kuona Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya  Jamii Zanzibar (ZSSF), ikiwekeza kwenye miradi mikubwa zaidi ikiwemo ya umeme. Alizungumza wakati wa kuzindua nyumba  za kisasa za bei nafuu  zilizojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar  (ZSSF), leo 23 Desemba 2025, eneo la Mombasa, Unguja zilizopewa jina la 'Mji wa Rais Hussein Mwinyi'. Dkt. Mwinyi, alisema kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii inatekeleza miradi mikubwa ulimwenguni. Alisema  ni vema wakajifunze nchi zingine wanafanyaje na akatoa mfano wa Malaysia, Singapore na Indonesia ambako miradi  yote mikubwa ya maendeleo inafanywa  kwa  uwekezaji wa mifuko ya jamii. "Mfano hivi sasa  Zanzibar kuna changamoto kubwa ya umeme hivyo ningependa  kuona mkiwekeza   kwenye miradi mikubwa ya maendeleo kama hiyo" alisema. Alibainisha kuwa  kukamilika kwa mradi huo w...

HBD DKT. MWINYI. DUA, VISOMO VYA WANAMICHEZO KILA KONA

Image
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar WANAMICHEZO Zanzibar wameandaa dua na  sadaka kwa ajili  ya siku  ya kumbukizi ya kuzaliwa Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein  Ali Mwinyi. Akizungumza kwa  niaba  ya wanamichezo  wa Zanzibar, mchambuzi wa michezo, Ally Rashid Pizaro alisema dua na sadaka vitafanywa viwanja vya ZBC, Unguja. "Wanamichezo wanashukuru kwa kazi kubwa aliyofanya  katika sekta ya michezo upande wa miundombinu na kumuombea dua kwa mambo makubwa zaidi anayoenda  kufanya  awamu hii inayofuata" alisema. Alisema wanamichezo wanamtakia Mwenyezi Mungu azidi azidi kumpa uadilifu na moyo wa kuwatumikia waZanzibari.  Ujenzi wa Kijiji cha AFCON, viwanja vya michezo jumuishi kila wilaya, ukarabati wa Uwanja wa Amaan ambao sasa ni New Amaan Complex na  Gombani Complex Pemba na vingine  ni sehemu  ya sababu  ya wanamichezo hao kuandaa dua na visomo kila kona, Unguja na Pemba.

WITO WA AMANI WATAWALA TAMASHA 'IJUKA OMUKA ' KAGERA

Image
 Na Mwandishi  Wetu, Kagera WITO wa amani umetawala Tamasha la kila mwaka la Ijuka Omuka (Kumbuka Nyumbani) ambako Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa, aliwapongeza viongozi wa dini na wananchi kwa kulinda amani ya mkoa wa Kagera. Fatma Mwassa alisema kama kiongozi wa serikali ataendelea kuwatumikia wanaKagera kwa kusimamia kikamilifu miradi yote ya maendeleo iliyoanzishwa. Mkuu huyo wa mkoa amewaahidi viongozi wa dini na wakazi wa Kagera kulitangaza na kulifanya tamasha hilo kuwa endelevu litakalowafanya wenyeji waishio ndani na nje ya nchi kuwa sehemu moja na kufanya uwekezaji wa pamoja. Awali, Shekhe wa Mkoa wa Kagera, akiwakilisha  Baraza Kuu la Waislamu  (BAKWATA), Haruna Kichwabuta alisema, Mkoa wa Kagera umepitia machungu mengi ikiwa ni pamoja na wakati amani ilipotoweka wakati wa uvamizi  wa Nduli Iddi Amin wa Uganda. "Kagera tumewahi kukumbwa na matukio mengine yaliyopoteza amani, hivyo kupoteza amani kwa mara nyingine ni kukumbushia machungu ya miaka i...

MBETO 'AMPASHA' OMO SIASA ZA HASAMA ZANZIBAR

Image
  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar  Chama cha Mapinduzi (CCM), kimemtaka Mwenyekiti  wa ACT Wazalendo  Othman Masoud  Othman kuacha porojo na kuwapotosha wananchi kwa kupandikiza maneno  ya hasama na chuki  katika jamii huku akiahidi mambo  yasiowezekana. Vile vile,  CCM kimesisitiza kuwa Uchaguzu Mkuu 2025 umemalizika, wananchi  wametumia haki yao ya kikatiba na kidemokrasia kwa kuiweka Serikali  walioitaka  madarakani. Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati  Maalum ya NEC  Zanzibar, Idara ya itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamisi  Mbeto Khamis aliyemtaka Othman kukubali ukweli    ameshindwa  uchaguzi kutokana na nguvu ya maamuzi ya wengi. Mbeto  alisema  Othman hana sababu zenye mashiko, bali  anajaribu  kuidanganya Dunia akidai  yeye ndiye mshindi wakati Tume  ya Uchaguzi  Zanzibar (ZEC), imeshamtangaza mgombea aliyeshinda Urais. Alisema Othman  asingeweza k...

Mbeto 'amvaa' Heche wa Chadema

Image
 Mwandishi Wetu, Zanzibar CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimebainisha kuwa hakuna uchaguzi utakaorudiwa wala serikali ya mpito itakayoundwa kama inavyodaiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), kwani taratibu zote zilifuatwa. Kupitia Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John   Heche chama hicho ambacho kilisusia uchaguzi mkuu uliopita hivi sasa kinadai kwenye vyombo vya habari na mitandao ya jamii, kuundwa serikali ya mpito, kuvunjwa Tume Huru ya Taifa Uchaguzi na kurudiwa uchaguzi mkuu uliopita 29 Oktoba 2025. Akizungumza mjini Unguja 16, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar. Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema serikali ya mpito huundwa pale kunapokuwa na tatizo mathalani Serikali au Tume ya Uchaguzi imekiondoa chama kwa mizengwe au madai ya kutoshindwa kihalali. Alisema mwenezi huyo kuwa kabla ya kufikia uchaguzi kuna hatua chama kinatakiwa kufuata na uchaguzi umefanyika, vyama 18 vimeshiriki na chama kimoja hakikushiriki na ndio ki...

DKT. NCHIMBI KAMPASI YA UDSM BUKOBA IWE KITOVU CHA UVUMBUZI

Image
  Mwandishi Wetu, Kagera Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), kimetakiwa kuhakikisha Kampasi Mpya ya Mkoa wa Kagera inakuwa kitovu cha uvumbuzi, ubunifu na mahali ambapo vijana watawezeshwa kuibua mawazo mapya. Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa kampasi hiyo katika kijiji cha Itahwa, wilayani Bukoba leo 15 Desemba 2025, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Nchimbi alisema pia chuo hicho kiwe sehemu ya kufanya ubunifu na kutumia fursa za soko la pamoja la Jumuia ya Afrika Mashariki. Dkt. Nchimbi alisema UDSM wana wajibu wa kuhakikisha mitaala itakayotumika katika kampasi hiyo inalenga moja kwa moja katika kuleta maendeleo ya jamii kwa kutoa zaidi elimu-ujuzi (Elimu ya amali) kwa kuwa mkoa wa Kagera na Kanda yote ya Ziwa zina fursa nyingi za kiuchumi. “Kwa kuwa mkoa wa Kagera unapakana na nchi jirani, uwepo wa kampasi hiyo utatoa fursa na kuvutia vijana katika nchi hizo kuja kujipatia maarifa muhimu” alisema na kuongeza kuwa kampa...

MHANDISI: DAR JENGENI UTAMADUNI WA KUHIFADHI MAJI

Image
 MHANDISI: MUWE NA UTAMADUNI WA KUHIFADHI MAJI Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam WAKAZI wa Dar es Salaam wametakiwa  kuwa na utamaduni wa kuhifadhi maji na kuyatumia kwa matumizi sahihi. Akizungumza wakati wa ziara ya kuangalia upatikanaji wa maji kama ratiba inavyoeleza katika wilaya ya Kinondoni, Kata ya Mwananyamala leo 15 Desemba 2025, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya  Maji Safi, Taka na Usafi wa Mazingira (Dawasa), Mhandisi Mkama Bwire alisema kwa sasa kinachofanyika kwa sasa ni kuhakikisha maji yanapatikana kulingana na ratiba inavyoeleza. Alisema mamlaka yake itaendelea kupita mitaani kuhakikisha maji hayo ya mgawo yanawafiki wateja majumbani kulingana na ratiba. Jiji la Dar es Salaam lipo katika mgawo wa maji kwa zaidi ya wiki mbili sasa hivyo kusababisha kuwepo mgawo huku maeneo mengine yakiwa  hayana kabisa huduma hiyo.

MAMIA WAMUAGA JENISTA MHAGAMA PAROKIANI PERAMIHO, RUVUMA

Image
 MAMIA WAMUAGA JENISTA MHAGAMA    PAROKIANI PERAMIHO, RUVUMA Na Mwandishi  Wetu, Ruvuma MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa  Peramiho, umeagwa leo 15 Desemba 2025  katika Kanisa   Katoliki la Mt. Benedict, Abasia ya Peramiho Jimbo Kuu, Songea. Ibada hiyo ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa  na serikali, Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba alisema baada ya Ibada ya kuaga alisema serikali itajitahidi watoto wa marehemu waweze kufikia ndoto zao kitaaluma. Mbunge huyo, anatarajiwa kuzikwa kesho 16 Desemba 2025, Kijiji cha Ruanda, wilaya  ya Mbinga, mkoani Ruvuma.

RAIS DKT. MWINYI ANAIJENGA ZANZIBAR YA MFANO DUMIANI-MBETO

Image
  RAIS DKT. MWINYI ANAJENGA ZANZIBAR YA MFANO DUNIANI-MBETO Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar   Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Uongozi katika ngwe ya pili chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi utaiachia Zanzibar alama zisizofutika kwa maendeleo  ya nchi na watu wake. Alama na zawadi hizo zitabaki kuwa kumbukumbu za kudumu za maendeleo ya Zanzibar. Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya  itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis,  ameeleza hayo mbele ya waaandishi wa habari ofisi kwake Kisiwandui Mjini Unguja.  Katika maelezo yake, Mbeto  alitaja ujenzi wa uwanja wa Ndege wa kisasa huko Pemba na barabara ya lami ya njia nne toka Chake Chake hadi Mkoani yenye urefu wa lilomita 45.3 mkoa wa Kusini Pemba.  Kadhalika Mbeto  alisema utafanyika ujenzi wa Kijiji cha Michuano ya Soka   ya Mataifa ya Afrika (AFCON) ambapo uwanja mkubwa wenye uwezo wa kuchukua zaidi ya washabiki 40 unajengwa Fumba, Mkoa wa Mjini Magha...

MWI.I WA JENISTA MHAGAMA WAWASI.I RUVUMA

Image
 MWILI WA JENISTA MHAGAMA WAWASILI RUVUMA Na Mwandishi Wetu, Songea MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, umewasili Mjini Songea Mkoani Ruvuma leo 14 Desemba 2025 na kupokewa na waomboleza wakiongozwa na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani humo. Mwili huo mara baada ya kuwasili ulipelekwa nyumbani kwake Mjini humo na unatarajiwa kuzikwa 16 Desemba 2025, Kijiji cha Ruanda, Mbinga mkoani Ruvuma.

DKT. NCHIMBI KUWEKA JIWE LA MSINGI TAWI UDSM BUKOBA

Image
  DKT. NCHIMBI KUWEKA JIWE LA MSINGI TAWI UDSM BUKOBA Na Mwandishi Wetu, Bukoba MAKAMU wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa tawi la Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), 15 Desemba 2025. Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mjini Bukoba , Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa alisema chuo hicho kitajengwa Kijiji cha Itahwa , Kata ya Kalagabaine , Halmashauri ya Mji wa Bukoba . Alisema Dkt. Nchimbi katika uwekaji wa jiwe hilo la msingi ataambatana na Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete . Alisema ujenzi wa chuo hicho ni sehemu ya mpango wa serikali kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu na kufungua fursa za kiuchumi kwa wenyeji na vitongoji vyake na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo muhimu. Awali akizungumza wakati wa mkutano huo, mratibu wa ujenzi wa chuo hicho, Profesa Liberato Haule alisema awamu ya kwanza ya ujenzi wa chuo hicho 2026/2027 utah...

ĎKT. NCHIMBI KUWEKA JIWE LA MSINGI TAWI UDSM BUKOBA

Na Mwandishi Wetu, Bukoba MAAMU wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa tawi la Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), 15 Desemba 2025. Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mjini Bukoba, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa alisema chuo hicho kitajengwa Kijiji cha Itahwa, Kata ya Kalagabaine, Halmashauri ya Mji wa Bukoba. Alisema Dkt. Nchimbi katika uwekaji wa jiwe hilo la msingi ataambatana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Alisema ujenzi wa chuo hicho ni sehemu ya mpango wa serikali kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu na kufungua fursa za kiuchumi kwa wenyeji na vitongoji vyake na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo muhimu. Awali akizungumza wakati wa mkutano huo, mratibu wa ujenzi wa chuo hicho, Profesa Liberato Haule alisema awamu ya kwanza ya ujenzi wa chuo hicho 2026/2027 utahusisha majengo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 800. “Chuo a...

Tafiti zitatue changamoto-Rais Dkt. Mwinyi

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amevihimiza vyuo vikuu Zanzibar, kuongeza kasi na kufanya tafiti nyingi zaidi zitakazosaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo 13 Disemba 2025 katika Mahafali ya 25 ya Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al Sumait, Chukwani, Mkoa wa Mjini Magharibi. "Ni muhimu tafiti zinazofanyika zitumike kuleta matokeo chanya na kuchangia maendeleo ya Taifa na jamii, badala ya kubakia bila kutumika" alisema. Alibainisha kuwa amefahamishwa kuna tafiti nyingi zimefanyika bila kutumika na kusambazwa kwa jamii, hali inayosababisha kushindwa kuchangia kikamilifu katika utatuzi wa changamoto zilizopo. Dkt. Mwinyi alisema tafiti zinazofanyika katika vyuo vikuu, zisipotumika hushusha hadhi ya chuo husika hivyo na kushindwa kuchangia maendeleo ya Taifa kama ilivyokusudiwa. Rais Dkt. Mwinyi alisema Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al Sumait katika...