CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na wakazi wa majumba ya Mjerumani Kikwajuni kwa kufikia maridhiano ambayo sasa yanatoa nafasi ya kuanza utekelezaji wa mradi ujenzi wa nyumba bora za kisasa ambazo zinatarajiwa kubadili mandhari ya Mji wa Unguja. Akizungumza na wanahabari waliofika ofisini kwake, leo 05 Machi 2026, CCM Kisiwandui kujua kinachoendelea kwenye mradi huo kutokana na kujitokeza sintofahamu baina ya baadhi ya wakazi na serikali, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema kufuatia maridhiano hayo mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani Milioni 45 sasa unaenda kutekelezwa. Alisema tayari Tsh.Bilioni 1.8 zimelipwa kwa wananchi waliokuwa wakiishi katika nyumba zilizopo katika maghorofa hayo yaliy...

Comments
Post a Comment