Mwandishi Wetu, Zanzibar CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakitamvumilia mteule yeyote wa Rais wa Awamu ya Nane, Dkt. Hussein Ali Mwinyi wala taasisi yoyote itakayoshindwa kusimamia utunzaji wa miundombinu ya kisasa inayojengwa Zanzibar kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Akitoa tathmini ya ziara inayoendelea ya Rais Dkt. Mwinyi ya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu wa Kamati Maalum NEC, Zanzibar Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema kote walipoenda katika ziara hiyo, Rais Dkt. Hussein Mwinyi anasisitiza utunzaji miundombinu. "CCM tunaunga mkono kauli yake na tunafuatilia na tunasisitiza kuwa hatutamvumilia mteule au mtendaji yeyote atakaye zembea kwenye eneo lake n...
Comments
Post a Comment