Posts

Showing posts from January, 2026

MBETO: NENDENI BUNGENI MKASIMAMIE MASLAHI YA ZANZIBAŔ

Image
                                            Na Mwandishi Wetu, Zanzibar WAJUMBE watano kutoka Baraza la Wawakilishi walioteuliwa kuiwakilisha Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametakiwa wakayasimamie maslahi ya Zanzibar kwa mujibu wa katiba na makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964. Akizungumza katika kipindi cha Safari ya Bahari kinachorushwa na Bahari FM , mjini Unguja, Zanzibar 28 Januari 2026 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema Wajumbe hao kutoka Baraza la Wawakilishi ambao wameenda kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano watambue wajibu wao kuwa ni kuitetea Zanzibar na sio wameenda huko kukaa kimya. "Wakajenge hoja za nguvu na sio nguvu za hoja kuhusiana na mgawanyiko wa raslimali za Taifa ikiwemo mikopo na misaada inayokuja kwa jina la Muungano wa Tanzania na pia sua...

MBETO: MIUNDOMBINU YA SOKA ZANZIBAR ITUMIKE KUTUNZA HISTORIA

Image
                                        Na Mwandishi Wetu Madrid, Spain MIUNDOMBINU ya michezo inayojengwa hivi sasa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi hususan soka inaweza kutumika kuhifadhi historia ya mchezo huo, wachezaji wa zama zote wa timu ya Taifa na kufanywa kuwa chanzo cha mapato kwa watu kutembelea kwa kulipa viingilio na sio kusubiria kunapokuwa na mechi pekee. Akizungumza wakati alipofanya ziara katika Uwanja wa Santiago Bernabue wa klabu ya soka ya Real Madrid nchini Spain, Katibu wa Kamati Maalum NEC, Zanzibar, Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema viwanja ni chanzo cha mapato hivyo wizara husika ijiandae kwa ajili ya kuutumia uwanja wa michuano ya AFCON 2027 kuiingizia serikali mapato na hata klabu pia watambue hilo kuwa viwanja ni vitega uchumi na pia ni sehemu ya kuhifadhi historia na jinsi gani miu...

UCHUMI WA KIDIJITALI NI KIPAUMBELE CHA ZANZIBAR

Image
                                           Na Mwandishi Wetu, Zanzibar Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), itaendelea kuweka kipaumbele kikubwa katika uendeshaji wa uchumi, utoaji wa huduma za Taasisi za Umma pamoja na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo ya kidigitali . Hayo yalisemwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar leo 26 Januari 2026, wakati alipokutana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Angellah Jasmine Kairuki , pamoja na watendaji wakuu wa Wizara hiyo. Dkt. Mwinyi katika mazungumzo hayo amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi itaendelea kuweka kipaumbele kikubwa katika uendeshaji uchumi, utoaji wa huduma za taasisi za umma pamoja na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo ya kidijitali. "Kuna umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara za Muungano na...

CCM YAMTEUA DKT. KOMBA UBUNGE PERAMIHO

Image
                                           Na Mwandishi Wetu, Zanzibar KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu  ya CCM Taifa imemteua Dkt. Lazaro Kilian Komba kuwa mgombea ubunge  Jimbo la Peramiho katika uchaguzi mdogo  unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu 2026 kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Jenister Mhagama lililopo Wilaya ya Songea  Vijijini, Mkoa wa Ruvuma. Kikao cha kamati  hiyo kimefanya  uteuzi huo kwa kuzingatia mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 105 (7)(f) ya Katiba ya CCM  ya Mwaka 1977 toleo la Julai 2025. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kiongosi, pia kamati hiyo imewachagua  wagombea  wa  nafasi mbalimbali  bungeni. "Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu CCM Taifa tarehe 25 Januari 2026 imepitia na kujadili kishja...

KAMATI KUU HALMASHAURI KUU CCM TAIFA YAKUTANA LEO ZANZIBAR

Image
 Leo tarehe 25 Januari, 2026 Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kimefanyika Zanzibar,  kikichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

SERIKALI KUMUENZI EDWIN MTEI KWA MIRADI YA MAENDELEO

Image
                                         Na Mwandishi Wetu, Arusha WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba , amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , katika Ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Edwin Mtei , akimtaja kuwa kiongozi mahiri, mzalendo na nguzo muhimu katika historia ya uchumi na demokrasia ya Tanzania. Akizungumza katika ibada hiyo iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Tengeru, Jijini Arusha , Dkt. Nchemba alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua mchango mkubwa wa marehemu kwa Taifa na Serikali mara zote itaenzi mchango wake mkubwa katika uchumi na demokrasia nchini. Waziri Mkuu alisema Mzee Mtei alikuwa miongoni mwa Watanzania wachache waliobahatika kuhudumu katika nyadhifa zote kuu za sekta ya fedha, ikiwemo kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Wazi...

DKT: MISIKITI IWE KITOVU CHA UTATUZI MIGOGORO JAMII

Image
                                             Na Mwandishi Wetu, Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuitumia misikiti kama vituo muhimu vya kujadili na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii, sambamba na kutoa ufumbuzi unaofaa kwa maendeleo ya jamii. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo 23 Januari 2026, baada ya kujumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa wa Mfereji wa Wima, Mkoa wa Mjini Magharibi. Amesema kuwa changamoto zilizopo katika jamii ni nyingi, hivyo ni wajibu wa waumini kushirikiana kupitia misikiti kwa kuhamasisha michango itakayosaidia familia na jamii duni zisizojiweza.  Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amepongeza uongozi wa Msikiti huo wa Mfereji wa Wima kwa kuanzisha na kuendesha utaratibu wa ukusanyaji wa...

WAZIRI KAIRUKI ASHUHUDIA MAONYESHO TEKNOLOJIA BUNIFU CHINA

Image
                                                Na Mwandishi Wetu, China Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Kairuki  amehudhuria maonyesho kiteknolojia bunifu zilizotengenezwa na Kampuni ya Huawei yaliyofanyika katika ukumbi wa Von Naumann, Jijini Shenzhan, China.                          Katika maonyesho hayo zilishuhudiwa teknolojia za kisasa ambazo ni pamoja na G5, Akili Unde, huduma za Wingu, ,miundombinu ya mawasiliano inavyotumika katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, madini, elimu, usafiri, bandari, huduma za kifedha na Miji Janja. Waziri Kairuki alisema Tanzania itaendeleza uhusiano uliokuwepo zaidi ya miaka 10 katika miradi ya TEHAMA ikiwemo upanuzi wa Mkongo wa Taifa, ujenzi wa Miundombimu vijijini na miradi ya uwajibikaji kwa jamii. Lengo la ushirikiano huo ali...

DC KARATU ATETA NA WAHADZABE,WADATOGA

Image
Na Mwandishi Wetu, Karatu KAMATI  ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karatu, ikiongozwa na  Mkuu wa Wilaya hiyo. Lameck Karanga, imekutana na baadhi ya wananchi wa kabila la Wahadzabe wao kiasili ni wawindaji na Wadatoga ambao ni wahunzi na wafua nyuma. Ziara hiyo ambayo imefanyika katika eneo la Eyasi wilayani humo ambako Wahadzabe linalofahamika kutokana na mila na silka zake za kiasili likiamini kuwa nyama ya nyani ndiyo nyama bora na tamu kuliko zote duniani na limekuwa likimtumia mnyama huyo kama kielelezo muhimu kwa maisha yao ya kila siku. Wadatoga bado wakiendelea kutumia zana za kale katika uhunzi wa kufua bidhaa mbalimbali za kitamaduni. Makabila yote mawili yanapatikana ndani ya Jiopaki ya Ngorongoro Lengai inayopatikana wilaya ya  Karatu,  Ngorongoro na Monduli, wilaya ambazo baadhi ya maeneo yake yanaunda Jiopaki ya kidunia inayojulikana kama  Ngorongoro Lengai  Global Geopark  inayotambuliwa kuwa ni Urithi wa Utamaduni na Shirika la Umoja ...

MKUTANO WA AFYA NORDIC, AFRIKA LEO STOCKHOLM

Image
                                   Na Mwandishi Wetu, Stockholm Sweden Uzinduzi wa Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Afya kati ya nchi za Afrika na Nordic (African–Nordic Health Summit, unafanyika leo 22 January 2026, Jijini Stockholm nchini Sweden, Tanzania ikiwakilishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi. Naibu huyo Waziri ambaye ameenda kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mohamed Omary Mchengerwa na amepokewa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Sweden na Balozi, Mobhare Matinyi  21 Januari 2026. Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya kundi la Mabalozi wa Afrika wanawake wa nchi za Nordic, The Maternity Foundation, Dalberg Media na Danish Alliance for Global Health, pamoja na wadau wengine wa kimataifa akiwemo Global Financing Facility, World Diabetes Foundation, Ferring Pharmaceuticals na Laerdal Global Health, lengo kuu ni kujadili masuala ya afya ya uzazi na mtot...

DKT. MWINYI AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI ZANZIBAR

Image
                                             Na Mwandishi Wetu, Zanzibar SERIKALI ya Mapinduzi imewahakikishia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwa itaendelea kuweka vivutio na mazingira bora ya uwekezaji kwa lengo la kunufaika na miradi yao. Akizungumza leo 20 Januari 2026 wakati wa uzinduzi wa Boti Mpya ya abiria ya Kilimanjaro 9 ‘Dragon of the Sea’, inayomilikiwa na Kampuni ya Azam Marine Ltd katika hafla iliyofanyika Mtoni Verde, Mkoa wa Mjini Magharibi. Rais Dkt. Mwinyi alisema serikali inaendelea kuimarisha sekta ya usafirishaji baharini kupitia ujenzi wa miundombinu ikiwemo bandari ya Fumba na bandari nyingine Unguja na Pemba hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi na kuboresha huduma za usafiri baharini. “Nakupongeza mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam, Mzee Said Salim Bakhresa kwa uwekezaji mkubwa unaogusa maisha ya wananchi” alisema na kuongeza kuwa Kamp...

WAZIRI KAIRUKI ATAKA UJUMUISHI WANAWAKE, VIJANA KIDIJITALI

Image
                                        Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki ambaye pia ni Mbunge wa Kibamba, anasema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kisera, kifedha na kitaasisi ili kuchochea uvumbuzi unaojenga ajira na kujitegemea kwa Taifa. Akizungumza wakati wa kufunga Kongamano la 9 la Mwaka 2026 la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TAIC 2026) 19 Januari 2026, Waziri Kairuki alisema serikali ina dhamira ya dhati kuhakikisha wanawake na wasichana wanashiriki kikamilifu katika mabadiliko ya kijigitali na uvumbuzi wa kiteknolojia. “Nimefurahi kuona jukwaa hili limetenga siku hii kwa ajili ya wanawake katika TEHAMA kwani wana mchango mkubwa katika kuiendeleza na kuanzisha bunifu na kuongoza taasisi za kijiditali” alisema. Alibainisha kuwa pia wana nafasi kubwa ya kubuni suluhisho zenye athari cha...

DKT. MWINYI MUUMINI WA UCHUMI WA KIDIGITALI

Image
                                              Na Mwandishi Wetu, Zanzibar Miaka mitano iliyopita, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati anaingia madarakani miongoni mwa vitu vya mwanzo kufanya ni kutekeleza ahadi yake ya mageuzi ya kiuchumi. Wananchi wake wanasema akitumia akili kubwa bila mabavu, kufoka majukwaani, kusukumana na wakandarasi site au kuvamia ofisi za umma na kutoa vitisho, Dkt. Mwinyi anafanya mageuzi. Mageuzi ambayo ndani ya miaka mitano iliyopita yamehuisha Pato la Ndani la Taifa (GDP), kutoka asilimia 3 za awali hadi 7.2 kwa mwaka 2025 huku matumizi ya Tehama yakitajwa kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji huo. Kulingana na taarifa ya hivi karibuni, uchumi wa Zanzibar umekua kwa asilimia 7.2 kutoka 3 za Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi Zanzibar (sasa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Fedha na Mipango),...