Posts

Showing posts from September, 2025

Dkt, Hussein Mwinyi akatiza kampeni kufuatia kifo cha kaka yake

Image
 

TANZIA: KAPTENI ABBAS MWINYI AFARIKI

Image
                 * T A A R I F A   Y A  MSIBA, M A Z I K O* Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt Hussein Ali Hassan Mwinyi anasikitika kutangaza kifo cha Kaka yake Rubani Abbas Ali Hassan Mwinyi aliyefariki leo, Alhamis Tarehe 25 Septemba 2025. Zanzibar.. Ibada ya kumsalia Marehemu itafanyika katika Msikiti wa Zanzibar ( جميع ) - *Msikiti wa Qaboos baada ya sala ya Ijumaa na baada ya hapo maziko yanafanyika Mangapwani katika eneo ambalo amezikwa Mzee Ali Hassan Mwinyi* - ambapo watu waliopo maeneo ya Mangapwani, Bumbwini, Fujoni na maeneo ya karibu watapata kutabaruku kabla ya kuzika. Visomo Msikitini vitaanza saa 4 asubuhi. *إنا لله وانا إليه راجعون*

Selfie na mkuu

Image
  Mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM ambaye pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi na timu yake wakipiga picha na mfanyabiashara, Suleiman Haji Makame alipotembelea sokoni hapo na kuzungumza na wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba, leo tarehe 24 Septemba 2025.  Rais Dkt. Mwinyi amewasili leo Pemba kuendelea na mikutano ya kampeni ya CCM.

Mbeto: Ni Zanzibar pekee Afrika wazee wote wanalipwa posho kila mwezi

Image
 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar Awamu ya nane chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na mgombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao 29 Oktoba 2025, ndio serikali pekee Afrika ambako wazee wote waliofikisha umri wa miaka 70 wanalipwa posho bila kujali iwapo ana pensheni ya kustaafu au la. Akizungumza na wanahabari, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema kwenye masuala ya ustawi wa jamii, Rais Dkt. Mwinyi amefanya mambo makubwa kuliko kiongozi yoyote, Afrika. Alisema awali waliofikisha miaka 70 waliopo mitaani na katika nyumba za kutunzia wazee wanalipwa TSh.40,000 kila mwezi na pesa hizo ni tofauti na TSh.50,000 ya pensheni kwa wastaafu ambayo awali ilikuwa TSh.20,000. "Ukikuta mtu huyo alikuwa mtumishi wa umma na sasa kastaafu anakula 90,000 kwa mwezi" alisema Mbeto. Alibainisha kuwa mzee kama huyo kama anayeishi nyumba za kulelea wazee za Sebuleni, L...

Kikao kamati wakuu wa nchi kuzuia na kudhibiti magonjwa Afrika (CDC)

Image
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania inasisitiza umuhimu wa mifumo endelevu ya ufadhili ili kuhakikisha uthabiti wa kukabiliana na dharura za afya ya umma barani Afrika.   Makamu wa Rais amesema hayo wakati akishiriki katika Mkutano wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Afrika (CDC) uliyofanyika pembezoni mwa Kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani.  Amesema Tanzania imedhamiria kuongeza ukusanyaji wa rasilimali za ndani, kuimarisha masuluhisho ya kibunifu ya ufadhili pamoja na kuunga mkono mipango ya kikanda ambayo inapunguza utegemezi wa misaada kutoka nje, na hivyo kuhakikisha kuwa vipaumbele vya afya vya Afrika vinashughulikiwa na serikali za Afrika.   Makamu wa Rais amesema uzalishaji wa ndani wa vifaa vya uchunguzi, matibabu, na bidhaa nyingine muhimu za matibabu ni muhimu katika kujitegemea kweye sekta ya afya. Alisema Tanz...

Tuzo za Mwanasoka Bora 2025

Image
 

Sekta ya Madini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Sekta ya madini imeendelea kuwa nguzo ya uchumi nchini ambapo katika mwaka 2022 sekta hiyo imekua kwa asilimia 10.9 na kufikia mchango wa asilimia 10.1 kwenye Pato la Taifa mwaka 2024, ikilinganishwa na asilimia 9.0 mwaka 2023. Ametoa kauli hiyo Leo (Jumatatu, Septemba 22, 2025) wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya Nane ya Teknolojia ya Madini Mkoa wa Geita, yaliyofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan. Amesema kuwa hatua hiyo imetokana na jitihada mbalimbali za Serikali ya awamu ya sita ikiwemo kuimarishwa kwa mifumo ya ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa biashara ya madini,  matumizi ya mifumo ya kielektroniki (online mining cadastre system), uwepo wa masoko ya madini na ufuatiliaji wa mikataba ya uwekezaji. "Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka kipaumbele katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwenye sekta ya madini ili rasilimali za madini zichangie kwa katika uk...

24 Hours Building Permits

Image
 Invest with confidence, build with speed! In Tanzania’s Special Economic Zones, time is never wasted. Thanks to the One-Stop Facilitation Centre (OSFC), investors can now obtain their building permits in just 24 hours a process that used to take weeks or even months. This fast-track service means your project won’t be slowed down by bureaucracy. Instead, you can stay on schedule, save costs, and begin operations sooner. From the moment you step in, OSFC ensures that your journey as an investor is smooth, efficient, and fully supported. Tanzania is not only opening doors for investors it’s making sure those doors open quickly.  #InvestInTanzania #SEZ #EPZ #OSFC #EaseOfDoingBusiness

Mkutano Mawaziri Jumuia Madola

Image
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo, akishiriki Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, pembezoni mwa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, unaofanyika jijini New York, Marekani.

Soko jipya la kisasa kujengwa Kinyasini

Image
 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar Mgombea wa Kiti cha Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuwajengea soko la kisasa wafanyabiashara wa Kinyasini pindi akichaguliwa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika 29 Oktoba 2025. Akizungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali wa Kinyasini, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Dkt. Mwinyi alisema hiyo ni ahadi yake kwao na alifanya hivyo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kampeni za chama hicho. Dkt. Mwinyi pia aliendelea na kampeni zake kwa kuzungumza na kusikiliza changamoto za vijana na wajasiriamali wa sekta ya utalii wa Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja na amewahakikishia kuwa serikali inalenga kuimarisha sekta ya utalii ili kuwanufaisha wananchi wengi zaidi kupitia Sera ya Utalii kwa Wote.