WAZIRI DKT. KIJAJI UWANDANI KUDHIBITI TEMBO
KUELEKEA siku ya Wanyamapori Duniani, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, yuko uwandani katika Pori la Akiba Mkungunero kuyafunga makindi ya Tembo Visukuma mawembi ili kufahamu muelekeo wao, kwa lengo la kuwazuia kuleta madhara kwa wananchi na mazao yao. Zoezi hili pia ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba ya kuwadhibiti Wanyamapori wakali na waharibifu husani Tembo.