Posts

Showing posts from March, 2026

RAIS DKT. SAMIA MGENI RASMI HARAMBEE UPANDIKIZAJI FIGO, ULOTO

Image
                                      Na Hassan Kimweri, WAF - Dodoma  Hospitali ya Benjamin Mkapa imepanga kufanya harambee kwa ajili ya kusaidia matibabu ya upandikizaji Uloto kwa watoto wenye ugonjwa wa Selimundu (sickle cell) na kusaidia matibabu ya upandikizaji Figo kwa wananchi wenye uhitaji,katika  kuelekea maadhimisho ya kutimiza miaka 10 ya hospitali hiyo.  Kauli hiyo imetolewa 31 Machi 2026 na  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Prof. Abel Makubi,wakati akiongea na wanahabari na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya miaka kumi ya Hospitali hiyo na kilele chake kimepangwa kufanyike 8 Mei 2026.  "Jambo hili tunalifanya Sisi Benjamin Mkapa  kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), matibabu ya upandikizaji Figo na Uloto yanahitaji gharama kubwa sana, hivyo ni vigumu  kwa Mtanzania wa kipato cha chini kumudu gharam...

SERIKALI YAKARIBISHA UWEKEZAJI TOKA UTURUKI

Image
                               Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaa, SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imewakaribisha wawekezaji kutoka Uturuki kuwekeza katika sekta za kimkakati zikiwemo miundombinu, nishati na kilimo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuharakisha maendeleo ya uchumi na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili. Wito huo umetolewa na Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati alipokutana na Balozi wa Uturuki nchini, Dkt. Bekir Gezer, akiambatana na ujumbe kutoka Benki ya EXIM ya Uturuki, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam. Alitoa wito wa Uturuki kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji hususan katika ujenzi wa vipande vya Lot 3 na Lot 4 vya Reli ya Kisasa (Standard Gauge Railway (SGR)), ambavyo Benki ya EXIM ya Uturuki imeonesha nia ya kufadhili, ikiwa ni vipande muhimu katika kuunganisha mtandao wa reli unaoendelea ku...

RAIS DKT. MWINYI, NYUMBA ZA WAHUDUMU AFYA, MASHINE YA MRI PEMBA

Image
                                        Na Mwandishi Wetu, Zanzibar WAKATI Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatimiza siku 100 madarakani, mashine ya Upigajipicha kwa Mwangi wa Sumaku (MRI) katika Hospitali ya Abdallah Mzee, wilaya ya Mkoani Kusini Pemba na nyumba za wahudumu wa afya katika hospitali za wilaya, vinatajwa kuleta mageuzi makubwa sekta ya afya, ambayo wananchi wanadai hawajawahi, wala kuyafikiria katika maisha yao. Rais Dkt. Mwinyi katika sekta hiyo licha ya kufanya mambo makubwa miaka mitano iliyopita lakini bado anaendelea kusogeza huduma hizo jirani na wananchi. Rais huyo ambaye anatekeleza na kuisimamia sera ya huduma za matibabu bila malipo kwa kila mZanzibari, amevunja na kujenga upya vituo vya afya na kuboresha huduma ili kulinda afya za wananchi wote, Unguja na Pemba. Ujenzi huo wa miundombinu ya afya pia umezingatia makazi ya wahudumu wa afya kwani kila Hospitali ya wil...

UWEKEZAJI TSH.BIL. 10 HOSPITALI BINAFSI WAIIBUA SERIKALI

Image
                               Na Shaban K. Juma, WAF – Dar es Salaam SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano, imepongeza Hospitali ya E.M ya Kigamboni kwa kuwekeza takribani Tsh.Bilioni 10 katika kuboresha huduma za afya, wakati wa uzinduzi rasmi huduma za kisasa za uchujaji damu (dialysis) pamoja na CT Scan, hatua itakayorahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wananchi. Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, ametoa pongezi hizo 27 Machi 2026 jijini Dar es Salaam akimwakilisha Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, katika hafla ya uzinduzi huo. Amesema uwekezaji huo unaimarisha mchango wa sekta binafsi kwenye kuboresha huduma za afya na kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi. Dkt. Samizi ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kushirikiana na Serikali na kuendeleza sekta ya afya. Serikali imeimarisha miundombinu, ime...

DKT. MWINYI ATAKA USHIRIKIANO KISEKTA MKUMBI-II

Image
                                       Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano madhubuti kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI-II), ili kufikiwa kwa haraka malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo 27 Machi 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, katika Mkutano wa Uhakiki wa Rasimu ya MKUMBI-II, ulioandaliwa na Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta za umma na binafsi. Rais Dkt. Mwinyi amebainisha kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inalenga kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kipato cha juu ifikapo mwaka 2050, i...

SHIRIKA LAPONGEZWA KUPUNGUZA ATHARI UWEKEZAJI

Image
                                       Na Mwandishi Wetu, Dàr es Salaam  WAZIRI wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar amesema, Tanzania itaendelea kuimarisha zaidi ushirikiano na Shirika la Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI) katika juhudi za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, Sambamba na kuvutia mitaji zaidi ya sekta binafsi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Warsha ya ATIDI kuhusu “Kuimarisha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Tanzania” iliyofanyika hoteli ya Hyatt Regency,  Balozi Omar alilisifu shirika hilo kwa mchango wake mkubwa katika kutoa huduma za kupunguza hatari za uwekezaji (de-risking), hatua inayowapa wawekezaji na taasisi za kifedha ujasiri wa kushiriki katika miradi mikubwa barani Afrika. “Tanzania inajivunia kuwa si tu mwanachama, bali pia ni miongoni mwa waanzili...

MBETO: CCM TUMEPOTEZA KIOO CHA UPATANISHI

Image
                                      Na Mwandishi Wetu, Zanzibar  Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kimemtaja aliyekuwa Waziri  wake wa Nchi  Ofisi ya Waziri  Mkuu Sera, Bunge na Uratibu,  William  Vangimembe Lukuvi,  amekuwa  kamusi iliosaidia kufafanua na kuelekeza kila alipohitajika kutoa ushauri katika mambo  ya msingi. CCM kimesema kiongozi huyo alikuwa  kiungo na kiraka kilichoziba lolote  katika nyakati  zote ngumu aidha kwa masuala ya Kisiasa, kiutendaji  na Kiutawala.  Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo,  Khamis Mbeto Khamis  ameeleza hayo kwa masikitiko, huzuni na fadhaa kufuatia kifo cha mwanasiasa huyo kilichotokea Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma jana 25 Machi 2026. Mbeto alisema Tanzania imepoteza kiongozi wake madhubuti, jasiri,  mzalendo na mshauri muh...

DKT. MWINYI AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMPUNI YA CHINA

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo  26 Machi amefanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Liaoning Fangda Group of Companies ya China. Ujumbe huo wa China katika mazungumzo hayo yaliyofanyika ukumbi wa mikutano Ikulu, yaliongozwa na Mwenyekiti wake, Bw. Ao Xinhua.

WILLIAM LUKUVI AFARIKI DUNIA

Image
 

SAYANSI, TEKNOLOJIA KIPAUMBELE UDSM, CHUO KIKUU VIENNA

Image
                                        Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam JAMHURI ya Muungano wa Tanzania imesisitiza kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Vienna  katika nyanja za sayansi na teknolojia, ikiwemo nishati ya jua, ili kuzalisha wataalamu wenye ujuzi kwa manufaa ya pande zote mbili. Hayo yameelezwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo UDSM (Taaluma), Profesa Rose Upor alipofanya mazungumzo na  Ujumbe wa Austria ulioongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya kisiasa, Balozi Dkt. Hannah Liko, ulipotembelea chuoni hapo 24 Machi 2026 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu kati ya Tanzania na Austria. Profesa Upor amesema ili kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo kati ya UDSM  na Chuo Kikuu cha Vienna, kuna umuhimu wa kuongeza ufadhili wa masomo katika kada mbalimbali pamoja na kubadilishan...

MUONGOZO BORA WA MAABARA KUIMARISHA HUDUMA VIPIMO VYA WAGONJWA

Image
                                  Na Emmanuel Malegi, WAF – Kilimanjaro MIONGOZO bora ndani ya maabara imetajwa kama chachu ya kusaidia ufanisi wa kazi ikiwemo huduma za vipimo  na utoaji majibu sahihi kwa haraka. Hayo yamesemwa Machi 23, 2026 na Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Epidemiolojia na udhibiti wa magonjwa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Vida Mmbaga wakati akifungua kikao kazi cha kuandaa mikakati ya upimaji wa vimelea vya magonjwa ya Dengue, Kimeta na Brucelosis kinachoendelea mkoani Kilimanjaro. Dkt. Vida amesema kuwepo kwa mikakati hiyo kunasaidia na kutoa miongozo kwa wataalam wa Maabara kutojifanyia vipimo kiholela kwa kutumia njia wanazopenda badala yake ufanisi wa kazi utapimwa kwa kufuata miongozo iliyowekwa. “Kuwepo kwa miongozo hii kutasaidia upimaji wa ufanisi wa kazi ikiwemo kuzuia, kukinga pamoja na kudhibiti magonjwa mbalimbali kwa ufanisi, hivyo miongozo hii inatakiwa kutolewa mape...

DKT. MWINYI: WAELIMISHENI WADAU MATUMIZI MATOKEO YA TAFITI

Image
                                         Na Mwandishi Wetu, Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameushauri uongozi wa Kituo cha Tafiti za Kiuchumi, Kijamii na Uchambuzi wa Sera Zanzibar (ZRCP) kuandaa mikutano na mijadala na wadau ili kuwaelimisha umuhimu wa kutumia matokeo ya tafiti katika utekelezaji wa majukumu yao. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 24 Machi 2026, alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho, Juma Reli, pamoja na ujumbe wake waliofika Ikulu, Zanzibar. Aidha, amebainisha umuhimu wa kufanya maboresho katika mifumo ya usajili wa malipo ya kidijitali ili kuimarisha muda na uwazi, hususan katika sekta ya umma, na kushauri kuangaliwa upya kwa sera, sheria na kanuni katika eneo hilo. Mkurugenzi Juma Hassan Reli, ameunga mkono mapendekezo hayo na kueleza kuwa kituo hicho kipo tayari kushirikiana na Serikali k...

DKT. NCHIMBI: LINDENI , TUNZENI VYANZO VYA MAJI

Image
                                    Na Ofisi ya Makamu wa Rais, Morogoro Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa wito kwa Mamlaka zinazohusika pamoja na Watanzania kwa ujumla kuweka kipaumbele katika utunzaji na ulinzi wa vya vyanzo vya maji ili kuweza kurithisha kizazi kijacho nchi inayofaa kuishi. Makamu wa Rais ametoa wito huo alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Maji kwa Mwaka 2026 na Siku ya Maji Duniani iliyofanyika katika Viwanja vya Mkwawa mkoani Morogoro 22 Machi 2 Amesema ni lazima kuangalia sana umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji kwa kufanya uwekezaji wa kimkakati ambao unaangalia kuvitunza na kuongeza vyanzo vya maji Halikadhalika, Makamu wa Rais ametoa rai kwa Wizara na Taasisi zote za Umma nchini kujenga mtandao wa ushirikiano katika kuzikabili kuzitatua...