MHANDISI: DAR JENGENI UTAMADUNI WA KUHIFADHI MAJI
MHANDISI: MUWE NA UTAMADUNI WA KUHIFADHI MAJI
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAKAZI wa Dar es Salaam wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuhifadhi maji na kuyatumia kwa matumizi sahihi.
Akizungumza wakati wa ziara ya kuangalia upatikanaji wa maji kama ratiba inavyoeleza katika wilaya ya Kinondoni, Kata ya Mwananyamala leo 15 Desemba 2025, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi, Taka na Usafi wa Mazingira (Dawasa), Mhandisi Mkama Bwire alisema kwa sasa kinachofanyika kwa sasa ni kuhakikisha maji yanapatikana kulingana na ratiba inavyoeleza.
Alisema mamlaka yake itaendelea kupita mitaani kuhakikisha maji hayo ya mgawo yanawafiki wateja majumbani kulingana na ratiba.
Jiji la Dar es Salaam lipo katika mgawo wa maji kwa zaidi ya wiki mbili sasa hivyo kusababisha kuwepo mgawo huku maeneo mengine yakiwa hayana kabisa huduma hiyo.

Comments
Post a Comment