MBETO: VYAMA VIHESHIMU KATIBA ZANZIBAR


                                           Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kinasema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa nafasi nyeti kwa uchumi wa Zanzibar kwa mawaziri wanne toka ACT Wazalendo ambao hata hivyo hadi sasa hawajashiriki kuunda Serikali ya Umoja wa kiTaifa   ( SUK ) kama Katiba ya Zanzibar inavyoelekeza.

Kulinga na Katiba ya Zanzibar chama kinachofuatia kwa wingi wa kura katika Uchaguzi Mkuu, hutoa Makamu wa Kwanza wa Rais na hupewa nafasi  za maWaziri kulingana na wingi wa Viti vya Wawakilishi walivyoshinda ndani  ya siku tisini.

Akizungumza katika ziara za Rais Dkt. Hussein Mwinyi ambazo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu Mkuu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema kutokana na unyeti wa wizara hizo ndio maana anataka waache masuala ya vyama bali waheshimu Katiba ya Zanzibar kwani mgawanyiko wa mawaziri ni takwa la Sheria ambayo inatambua uwepo SUK.

Alisema suala la SUK ni la kikatiba sio matakwa ya vyama vya siasa hivyo ACT Wazalendo wanapaswa kuiheshimu na kuifuata na kikubwa wizara nne nyeti zipo wazi hadi sasa hazina mawaziri.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA