Tafiti zitatue changamoto-Rais Dkt. Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amevihimiza vyuo vikuu Zanzibar, kuongeza kasi na kufanya tafiti nyingi zaidi zitakazosaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo 13 Disemba 2025 katika Mahafali ya 25 ya Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al Sumait, Chukwani, Mkoa wa Mjini Magharibi.

"Ni muhimu tafiti zinazofanyika zitumike kuleta matokeo chanya na kuchangia maendeleo ya Taifa na jamii, badala ya kubakia bila kutumika" alisema.

Alibainisha kuwa amefahamishwa kuna tafiti nyingi zimefanyika bila kutumika na kusambazwa kwa jamii, hali inayosababisha kushindwa kuchangia kikamilifu katika utatuzi wa changamoto zilizopo.

Dkt. Mwinyi alisema tafiti zinazofanyika katika vyuo vikuu, zisipotumika hushusha hadhi ya chuo husika hivyo na kushindwa kuchangia maendeleo ya Taifa kama ilivyokusudiwa.


Rais Dkt. Mwinyi alisema Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al Sumait katika kuandaa wataalamu wa fani mbalimbali na kwamba itaendelea kuunga mkono juhudi hizo.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA