BALESI KOCHA MPYA KMC


 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TIMU ya Soka ya KMC, imemtangaza Abdallah Mohamed Juma 'Balesi' kuwa kocha mkuu wa timu hiyo inayosua sua katika Ligi Kuu ya NBC.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa uongozi wa timu hiyo kuachana na aliyekuwa kocha mkuu, Marcio Maximo.

Akitangaza hatua hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, Meya Songoro Mnyonge  alisema wameamua kuachana na Maximo kutokana na mwenendo wa matokeo yasiyoridhisha.

"Malengo na mkakati ya halmashauri ni kuwa na matokeo makubwa haikuweza kutimia sio kwamba kocha hakuwa mzuri ila alikuwa na malengo ya muda mrefu hivyo tukaamua kuachana nae" alisema Songoro.

Mkurugenzi wa Manispaa Kinondoni, Hanifa Suleiman Hamza alisema kuwa Manispaa Kinondoni imeamua kufanya uwekezaji mkubwa hivyo inafanya maboresho yanayofanana na thamani ya uwekezaji ndio maana wakaamua   kubadili upepo kwa kumchukua kocha mwingine kuendeleza timu.

Kocha Balesi alisema ana uzoefu wa majukumu ya aina  hiyo na sehemu zote alizopita katika mazingira kama hayo na alifanikiwa.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA