WIZARA YA ELIMU YAUKANA WARAKA


 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imekanusha taarifa zilizosambazwa mtandaoni kuwa shule hazitafunguliwa Januari na kueleza kuwa ratiba za mihula ya masomo ipo kama ilivvyopangwa.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo  cha Mawasiliano ya Serikali, Sylivia Lupembe ilisema shule za Awali, Msingi na Sekondari zitafunguliwa 13 Januari 2026.


"Tunapenda kuufahamisha umma wa waTanzania na wadau wote wa elimu ratiba ya mihula imeshatolewa na wizara kupitia Waraka wa elimu namba 5 wa 2025 na Waraka namba 6 wa mwaka 2025 kuhusu mihula ya masomo zilizotolewa 19 Novemba 2025 kuzingatia kalenda hiyo" ilisema taarifa hiyo.


Taarifa hiyo imewataka wananchi kulipuuza tangazo hilo na kuzingatia kalenda iliyotolewa awali na wizara.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA