HBD DKT. MWINYI. DUA, VISOMO VYA WANAMICHEZO KILA KONA
WANAMICHEZO Zanzibar wameandaa dua na sadaka kwa ajili ya siku ya kumbukizi ya kuzaliwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Akizungumza kwa niaba ya wanamichezo wa Zanzibar, mchambuzi wa michezo, Ally Rashid Pizaro alisema dua na sadaka vitafanywa viwanja vya ZBC, Unguja.
"Wanamichezo wanashukuru kwa kazi kubwa aliyofanya katika sekta ya michezo upande wa miundombinu na kumuombea dua kwa mambo makubwa zaidi anayoenda kufanya awamu hii inayofuata" alisema.
Alisema wanamichezo wanamtakia Mwenyezi Mungu azidi azidi kumpa uadilifu na moyo wa kuwatumikia waZanzibari.
Ujenzi wa Kijiji cha AFCON, viwanja vya michezo jumuishi kila wilaya, ukarabati wa Uwanja wa Amaan ambao sasa ni New Amaan Complex na Gombani Complex Pemba na vingine ni sehemu ya sababu ya wanamichezo hao kuandaa dua na visomo kila kona, Unguja na Pemba.

Comments
Post a Comment