Na Mwandishi Wetu, Zanziba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar ina kila sababu ya kuendeleza ushirikiano na uhusiano wa muda mrefu baina yake na Ireland. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 30 Aprili 2026, alipokutana na Balozi Nicola Brennan anayeiwakilisha Ireland nchini, aliyefika Ikulu, Zanzibar kwa mazungumzo maalum. _ Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, akiwa katika mazungumzo na mgeni wake, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Nicola Brennan, Ikulu Zanzibar. _ Rais Dkt. Mwinyi ameihakikishia Ireland kuwa Zanzibar itaendelea kuendeleza na kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na maendeleo, ustawi wa jamii, biashara na uwekezaji kwa manufaa ya nchi hizo mbili rafiki. Aidha, ameeleza kuwa uhusiano baina ya nchi hizo, ...