TUME KUTATHIMINI FIDIA MIRADI SMZ
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ameunda Tume ya Watu nane kupitia na kutathmini masuala ya fidia kufuatia utekelezaji miradi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Unguja na Pemba.
Taarifa kwa vyombo vya habari leo 31 Desembaa 2025 na kusainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Raqey Mohamed ilisema tume hiyo itakuwa na jukumu la kupitia masuala ya fidia na changamoto zilizojitokeza na kuishauri serikali kuchukua hatua stahiki.
Taarifa hiyo imewataka wananchi kuipa ushirikiano tume hiyo pindi itakapofika maeneo husika kwa ajili ya kupata taarifa stahiki kuhusiana na kazi walizopangiwa.
Tume inaundwa na wabobezi katika fani tofauti ambao ni pamoja na Salim Othman Simba ambaye ni mtumishi wa umma mstaafu na mtaalam wa Uthamini.
Yupo pia Mussa Kombo Mrisho, Mwanasheria, Ofisi ya Rais Ikulu. Khamis Muhidin Bakari, Mhandisi Viwanja vya Ndege Zanzibar na Fauzia Sindi Hassan Msajili katika Bodi ya Usajili wa Wakandarasi Zanzibar.
Wenginer ni Sabrina Yussuf Shaaban Mtaalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Ikulu Zanzibar, Mwanaidi Seleman Ali, mtaalam wa Sayansi ya Jamii katika Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchimi na Ramadhan Nassoro Mwinyi Mtaalam wa Fedhja na Uwekezaji kutoka Sekta Binafsi na Mzee Abdallah Khatib Mtalaam wa Masuala ya Umma ambaye pia anatoka sekta binafsi.

Comments
Post a Comment