Posts

Showing posts from May, 2026

MELI YA KWANZA YA KIMATAIFA YASHUSHA SHEHENA YA MAFUTA BANDARI JUMUISHI, MANGAPWANI ZAANZIBAR

Image
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar MELI ya kwanza kubwa ya mafuta ya Kimataifa kutoka Saudi Arabia yenye jumla ya lita Milioni 36 za mafuta ya ndege, petroli na dizeli yamewasili katika Bandari Jumuishi ya Mangapwani, Zanzibar. Kuwasili kwa meli hiyo moja kwa moja toka nje ya nchi, sasa kunaiondolea Zanzibar utegemezi wa mafuta yaliyokuwa yakishushwa bandari ya Tanga na kuletwa na meli ndogo Zanzibar jambo ambalo pia lilikuwa linaiongezea gharama ya uchukuzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). Akizungumza kuhusiana na kuwasili kwa shehena hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini Joseph Kirangi alisema kuwasili kwa meli hiyo na kushusha mafuta moja kwa moja Zanzibar ni kutokana na kuimarika kwa miundombinu ya uhifadhi wa raslimali hiyo muhimu kwa uchumi wa Zanzibar. Alisema hatua hiyo inatokana na dhamira ya dhati ya Rais wa Awamu ya Nane Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kuifanya bandari hiyo kuwa jumuishi kwa bidhaa mbalimbali ikiwemo nishati ya mafuta. Kirangi alisema kitambo Zanzibar...

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA MAENDELEO MIRADI YA UWEKEZAJI BAGAMOYO

Image
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uwekezaji katika Kongani ya Viwanda ya Bagamoyo baada ya kufanya matembezi na ukaguzi wa miradi inayosimamiwa na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) katika eneo la Bagamoyo Eco-Maritime City (BEMC), mkoani Pwani 30 Mei, 2026. Ziara hiyo ililenga kufahamu hali ya uendelezaji wa eneo hilo la uwekezaji pamoja na kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ambayo tayari imeanza kutekelezwa ndani ya eneo hilo la kimkakati. Bagamoyo Eco-Maritime City (BEMC) ilitangazwa rasmi kupitia Gazeti la Serikali Na. 123 la tarehe 24 Mei 2013 na ina ukubwa wa hekta 9,800, ambapo hekta 887 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Kisasa ya Mbegani.  Mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati inayolenga kuimarisha uwekezaji, maendeleo ya viwanda na biashara nchini. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa ...

TANZANIA, CHINA WAINGIA MAKUBALIANO UBORESHAJI HUDUMA ZA AFYA NCHI

Image
 Na Hassan Kimweri, WAF - Kagera  JAMHURI ya Muungano wa Tanzania na China zimefikia muafaka wa kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya kwa lengo la kuboresha huduma za tiba, tafiti, mafunzo ya wataalamu wa afya na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe amesema hayo 30 Mei 2026 ambapo makubaliano hayo yametokana na mazungumzo yaliyofanyika kati ya Waziri wa Afya, Mohammed Mchengerwa na wa China, Haichao Lei wakati wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), uliofanyika Geneva, Uswisi. Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China tumekubaliana wataalamu wetu waandae andiko dhana na mpango wa utekelezaji kwa kuanzia na uboreshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera pamoja na utanuzi wa huduma za upasuaji wa moyo kwa watoto JKCI, makubaliano haya yatasaidia uboreshwaji wa huduma kwa wananchi," alisema Dkt. M Alibainisha kuwa maeneo makuu ya ushirikiano ni pamoja na kuimarisha huduma za rufaa kat...

DIASPORA UFARANSA WATAKIWA KUCHANGIA MAENDELEO NCHINI

Image
 Na Mwandishi Wetu, Paris BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, Saidi Othman Yakubu, amezungumza na viongozi wapya wa Chama cha Watanzania Waishio Ufaransa (Diaspora Tanzania France) kujadili nafasi ya diaspora katika kuchangia maendeleo ya Taifa. Akizungumza na viongozi hao katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa katika Jiji la Paris, Balozi Yakubu amewapongeza kwa kuaminiwa kuongoza jumuiya hiyo na kusisitiza kuwa Serikali inathamini mchango wa diaspora katika maendeleo ya Taifa. Alisema kuwa utaalamu na uzoefu wa Watanzania waishio nje ya nchi ni rasilimali muhimu katika kukuza uwekezaji, biashara, utalii na uhamishaji wa maarifa. Balozi Yakubu alosema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayochochea ushiriki wa diaspora katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Balozi huyo pia amewahimiza kutumia nafasi zao za kitaaluma, kijamii na kiuchumi kuitangaza Tanzania kimataifa, sambamba na kuhamasisha fursa za uwekezaji, biashara na utalii zilizopo n...

SERIKALI, WADAU WAPANIA MALENGO KIMATAIFA HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO

Image
                          Na Hassan Kimweri, WAF - Dar es Salaam MGANGA Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe, amesema Serikali itaendelea kuhakikisha kila mama na mtoto mchanga wanapata huduma bora, salama na zenye viwango kupitia uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini na kufikia malengo ya Kimataifa.  Dkt. Magembe amesema hayo Mei 28, 2026 katika hafla fupi iliyofanyika katika hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam ya kupokea na kukabidhi vifaa tiba ikiwemo magari mawili yatakayosaidia huduma za mama na mtoto nchini.  "Serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya kazi kwa wahudumu wa afya pamoja na kuongeza uwezo wa wakunga ili kuhakikisha huduma za afya ya uzazi na mtoto zinawafikia wananchi kwa ubora unaotakiwa," amesema Dkt. Magembe  Aidha, Dkt. Magembe amesema kuwa ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo umeendelea kuleta matokeo chanya katika sekta ya afya, hususan katika kubores...

HOTELI DAR ZAFANYIWA TATHMINI KUELEKEA AFCON 2027

Image
                                   Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo amekutana na timu maalum iliyoundwa na wizara hiyo iliyoanza kufanya tathmini ya ubora wa hoteli na kuzipangia madaraja ikiwa ni maandalizi ya Afcon 2027. Akizungumza na wataalam hao walioanza kazi hiyo jijini Dar es Salaam na ambao watakwenda mikoa mbalimbali nchini kutathmini na kuzipanga hoteli katika madaraja, Dkt. Abbasi amesema zoezi hilo ni muhimu ili maeneo hayo yawe tayari kupokea wageni na kuwapa si tu huduma bali pia mandhari bora. “Mimi nimekaa kule michezo kwa muda kidogo nawajua aina ya mashabiki wanaokuja katika Afcon. Tutarajie wanakuja nchini watu wanaopenda vitu vizuri na huduma nzuri sasa hiyo ikichangika na matokeo ya uwanjani mtu kafungwa au kashinda vyote vinamfanya akirudi hotelini ahitaji ubora wa juu wa huduma lakini mandhari yenyewe ya ...

WAFANYAKAZI WIIZARA YA FEDHA WASISITIZIWA MAADILI, UBUNIFU

Image
Na Mwandishi Wetu, Dodoma WAFANYAKAZI, Wizara ya Fedha wametakiwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali ya Serikali ili kuimarisha utawala na utoaji huduma bora kwa wananchi. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula wakati akifungua rasmi Mkutano wa 39 wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kwa mwaka 2025/26 uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage (Treasury Square)  jijini Dodoma. Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar, Naibu huyo alisema kuna umuhimu kwa watumishi kuwa wabunifu, kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na ushirikiano ili kuongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa na Wizara na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya mawasiliano na mrejesho kwa wadau mbalimbali ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali. Luswetula, amewataka watumishi kuzingatia afya zao kwa kushiriki katika programu za upimaji wa afya zinazoratibiwa na Wizara, ku...

SMZ, SMT KUENDELEA KUKABILI ATHARI ZA KIUCHUMI

Image
Na Mwandishi Wetu, Pemba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na ya Jamhuri ya Muungano (SMT), zitaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na athari za kiuchumi zinazojitokeza kutokana na mgogoro wa vita vya Mashariki ya Kati, hususan kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, 27 Mei 2026, katika Baraza la Eid lililofanyika katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi, Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba. Amefahamisha kuwa hali inayoendelea Mashariki ya Kati inaleta madhara makubwa kiuchumi na kusababisha ugumu wa maisha kwa wananchi, hivyo Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha inapunguza athari zinazotokana na mgogoro huo. Aidha, amewaomba wananchi kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na hali hiyo, pamoja na kuwahimiza kuombea amani na kufikiwa kwa maelewano kwa ajili ya ustawi wa watu wote duniani. Akizu...

BALOZI OMAR AHUDHURIA UFUNGUZI MKUTANO WA MWAKA AfDB, CONGO BRAZZAVILLE

Image
Na Mwandishi Wetu, Congo Brazzaville WAZIRI wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, ameshiriki halfa ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 61 wa mwaka 2026 wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkutano Mkuu wa 52 wa Mwaka wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kintélé, katika Jiji la Brazzaville, Jamhuri ya Kongo. Katika ufunguzi huo, ujumbe wa Serikali ya Tanzania uliongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba. Mkutano huo wenye kauli mbiu ya "Kuhamasisha Ufadhili wa Maendeleo ya Afrika kwa Wingi katika Dunia Iliyogawanyika”, kauli ambayo inasisitiza umuhimu wa kuziba pengo la kifedha linalokua kwa mahitaji ya maendeleo ya Afrika, hasa katika mazingira ya kisiasa na kiuchumi duniani yanayobadilika kwa kasi. Zaidi ya wajumbe 3,000 kutoka nchi mbalimbali za Afrika na za mabara mengine ulimwenguni, zinashiriki mkutano huo, wakiwemo Marais na Wakuu wa Serikali za Afrika...