MKUTANO WA AFYA NORDIC, AFRIKA LEO STOCKHOLM


                                   Na Mwandishi Wetu, Stockholm Sweden

Uzinduzi wa Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Afya kati ya nchi za Afrika na Nordic (African–Nordic Health Summit, unafanyika leo 22 January 2026, Jijini Stockholm nchini Sweden, Tanzania ikiwakilishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi.

Naibu huyo Waziri ambaye ameenda kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mohamed Omary Mchengerwa na amepokewa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Sweden na Balozi, Mobhare Matinyi  21 Januari 2026.

Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya kundi la Mabalozi wa Afrika wanawake wa nchi za Nordic, The Maternity Foundation, Dalberg Media na Danish Alliance for Global Health, pamoja na wadau wengine wa kimataifa akiwemo Global Financing Facility, World Diabetes Foundation, Ferring Pharmaceuticals na Laerdal Global Health, lengo kuu ni kujadili masuala ya afya ya uzazi na mtoto.

Pia pamoja na mambo mengine, utajadili mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza na utawakutanisha viongozi wa Serikali kutoka nchi za Afrika na Nordic, watu mashuhuri, wafanyabiashara pamoja na asasi za kiraia.



Comments