CCM YAMTEUA DKT. KOMBA UBUNGE PERAMIHO
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imemteua Dkt. Lazaro Kilian Komba kuwa mgombea ubunge Jimbo la Peramiho katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu 2026 kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Jenister Mhagama lililopo Wilaya ya Songea Vijijini, Mkoa wa Ruvuma.
Kikao cha kamati hiyo kimefanya uteuzi huo kwa kuzingatia mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 105 (7)(f) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 toleo la Julai 2025.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kiongosi, pia kamati hiyo imewachagua wagombea wa nafasi mbalimbali bungeni.
"Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu CCM Taifa tarehe 25 Januari 2026 imepitia na kujadili kishja kufanya uteuzi wa wagombea uongozi wa CCM wanaotokana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Inawataja wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa wanaotokana na Bunge toka Bara (nafasi 3) kuwa ni Paul Makonda na Livingstone Lusinde wakati wanawake (nafasi 1) ni Asia Abdulkarim Halamga.
Wanaotokana na Bunge Zanzibar (nafasi 2) ambao ni Khamis Mussa Omary na wanawake ni Tauhida Cassian Galos na Katibu wa Wabunge wote (nafasi 1) ameteuliwa Agnes Elias Hokororo.
Wenyeviti wa Bunge (nafasi 3) nao ni Najma Murtaza Giga, Deodatus Philipo Mwanyika, Cecilia Daniel Pareso pia kamati hiyo imefanya uteuzi wa wagombea uongozi CCM wanaotokana na Baraza la Wawakilishi.
Wanaume (nafasi 2) ni pamoja na Said Ali Juma, Hamza Hassan Juma na wanawake (1), Lela Mohammed Mussa.
Wawakilishi wa CCM wanaoingia Bungeni kwa Mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaume (nafasi 3), Bakar Hamad Bakari, Dkt. Shahame Ali Ali na Simai Mohamed Said wakati wanawake (nafasi 1), Fatma Ramadhan Mandoba na Katibu wa Wawakilishi wote (nafasi 1), Machano Othmam Said.
Wenyeviti Baraza la Wawakilishi (nafasi 1) ni Mahmoud Omary Hamad na Udhaima Mbarak Tahir.

Comments
Post a Comment