MBETO: NENDENI BUNGENI MKASIMAMIE MASLAHI YA ZANZIBAŔ


                                            Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

WAJUMBE watano kutoka Baraza la Wawakilishi walioteuliwa kuiwakilisha Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametakiwa wakayasimamie maslahi ya Zanzibar kwa mujibu wa katiba na makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964.

Akizungumza katika kipindi cha Safari ya Bahari kinachorushwa na Bahari FM, mjini Unguja, Zanzibar 28 Januari 2026 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema Wajumbe hao kutoka Baraza la Wawakilishi ambao wameenda kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano watambue wajibu wao kuwa ni kuitetea Zanzibar na sio wameenda huko kukaa kimya.

"Wakajenge hoja za nguvu na sio nguvu za hoja kuhusiana na mgawanyiko wa raslimali za Taifa ikiwemo mikopo na misaada inayokuja kwa jina la Muungano wa Tanzania na pia suala la elimu ya juu" alisema Mbeto.

Alisema kuwa ni wengi katika Baraza la Wawakilishi waliomba nafasi hizo lakini hawakupata na kulingana na mgawanyiko ulivyo, Wawakilishi wanne wametoka CCM na mmoja ACT Wazalendo hivyo amewataka wakasimamie maslahi ya Zanzibar na kuhakikisha yanapatikana kwa wakati.

Alisema Mwakilishi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mbunge kamili na Rais anaweza kumteua kuwa Waziri Bara, hivyo ni vema watambue kuwa kuna mambo mengi wanayopaswa kuzungumzia kuhusu Zanzibar na Jamhuri ya Muungano kwa jumla.

" Waende wakawakishe vema, watu hawajui, wakiona kitu kinaletwa Zanzibar wanadhani tumepewa sadaka, ile ni haki ya Zanzibar na ipate kwa mujibu wa makubaliano ya Muungano kuhusiana na mgawanyo wa raslimali" alisema Mwenezi Mbeto.

Alisema Wawakilishe hao wamechaguliwa kulingana na Katiba ya CCM na alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa siku yake ya mfanano ya kuzaliwa na kumtakia afya njema na kitendo cha kuamua kupanda miti kuna nia njema ya kuiweka vema haiba ya nchi kwani miti ni uhai.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA