UCHUMI WA KIDIJITALI NI KIPAUMBELE CHA ZANZIBAR
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), itaendelea kuweka kipaumbele kikubwa katika uendeshaji wa uchumi, utoaji wa huduma za Taasisi za Umma pamoja na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo ya kidigitali.
Hayo yalisemwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar leo 26 Januari 2026, wakati alipokutana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Angellah Jasmine Kairuki, pamoja na watendaji wakuu wa Wizara hiyo.
Dkt. Mwinyi katika mazungumzo hayo amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi itaendelea kuweka kipaumbele kikubwa katika uendeshaji uchumi, utoaji wa huduma za taasisi za umma pamoja na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo ya kidijitali.
"Kuna umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara za Muungano na Zanzibar, hususan katika kuharakisha ujenzi wa Kituo cha Ukusanyaji wa Taarifa (Data Centre) Zanzibar, kuboresha miundombinu ya mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa intaneti ya kasi" alisema Dkt. Mwinyi.
Waziri, Angellah Kairuki amemhakikishia ushirikiano wa karibu na Zanzibar ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano zilizo salama, za uhakika na zenye viwango vya kitaifa na kimataifa.





Comments
Post a Comment