DC KARATU ATETA NA WAHADZABE,WADATOGA


Na Mwandishi Wetu, Karatu

KAMATI  ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karatu, ikiongozwa na  Mkuu wa Wilaya hiyo. Lameck Karanga, imekutana na baadhi ya wananchi wa kabila la Wahadzabe wao kiasili ni wawindaji na Wadatoga ambao ni wahunzi na wafua nyuma.

Ziara hiyo ambayo imefanyika katika eneo la Eyasi wilayani humo ambako Wahadzabe linalofahamika kutokana na mila na silka zake za kiasili likiamini kuwa nyama ya nyani ndiyo nyama bora na tamu kuliko zote duniani na limekuwa likimtumia mnyama huyo kama kielelezo muhimu kwa maisha yao ya kila siku.

Wadatoga bado wakiendelea kutumia zana za kale katika uhunzi wa kufua bidhaa mbalimbali za kitamaduni.

Makabila yote mawili yanapatikana ndani ya Jiopaki ya Ngorongoro Lengai inayopatikana wilaya ya  Karatu,  Ngorongoro na Monduli, wilaya ambazo baadhi ya maeneo yake yanaunda Jiopaki ya kidunia inayojulikana kama  Ngorongoro Lengai  Global Geopark  inayotambuliwa kuwa ni Urithi wa Utamaduni na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO).

Akizungumza na jamii ya makabila hayo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Karanga amewapongeza wananchi hao kwa kuendelea kutumisha mila na tamaduni za asili huku wakiwa kielelezo katika utunzaji wa amani na utulivu katika maeneo yao na kuwataka kuendelea kuwa kielelezo bora cha jamii nchini kwani serikali itaendelea kuwalinda na kuboresha shughuli za utalii katika eneo hilo.

Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya jamii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Joas Makwati  ameeleza kuwa mradi wa Jiopaki ya Ngorongoro unanufaisha jamii zinazokaa ndani na nje ya eneo la hifadhi hiyo kwa kuwa shughuli za  ufugaji, uwindaji na kilimo hutegemea uwepo wa maji na uhifadhi wa misitu ya Ngorongoro.

Kabila la wahadzabe linaloishi pembezoni mwa eneo la Eyasi limekuwa likisifika kutokana na utaalam wake wa kuchoma na kula nyama za nyani jambo ambalo limewafanya wageni kutoka ndani na nje ya nchi kuwatembelea ili kuona jinsi mnyama huyo alivyokuwa tunu kwa kabila hilo.

Nyama ya nyani iliyochomwa vizuri kwa mujibu wa kabila hilo ina vionjo vitamu kutokana na nyani  kula mizizi, matunda na mimea pori ambayo huifanya nyama yake kuwa  na ladha ya kuvutia na yenye kuufanya mwili uweze kuhimili magonjwa mbalimbali.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA