DKT. MWINYI AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI ZANZIBAR
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi imewahakikishia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwa itaendelea kuweka vivutio na mazingira bora ya uwekezaji kwa lengo la kunufaika na miradi yao.
Akizungumza leo 20 Januari 2026 wakati wa uzinduzi wa Boti Mpya ya abiria ya Kilimanjaro 9 ‘Dragon of the Sea’, inayomilikiwa na Kampuni ya Azam Marine Ltd katika hafla iliyofanyika Mtoni Verde, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Dkt. Mwinyi alisema serikali inaendelea kuimarisha sekta ya usafirishaji baharini kupitia ujenzi wa miundombinu ikiwemo bandari ya Fumba na bandari nyingine Unguja na Pemba hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi na kuboresha huduma za usafiri baharini.
“Nakupongeza mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam, Mzee Said Salim Bakhresa kwa uwekezaji mkubwa unaogusa maisha ya wananchi” alisema na kuongeza kuwa Kampuni hiyo imewekeza Dola za Marekani Milioni 150 na kutoa ajira 281.
Mtendaji Mkuu wa Azam, Aboubakar Aziz alisema boti hiyo iliyotengenezwa China ina uwezo wa kubeba abiria 631 na ina mifumo ya kisasa ya kulinda mazingira bahari.
Upande mwingine, Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Saleh Saad Muhammed alisema hadi sasa miradi ya uwekezaji yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 6.8 imesajiliwa ikitoa ajira 28,000 za moja kwa moja.





Comments
Post a Comment