WAZIRI KAIRUKI ASHUHUDIA MAONYESHO TEKNOLOJIA BUNIFU CHINA
Na Mwandishi Wetu, China
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Kairuki amehudhuria maonyesho kiteknolojia bunifu zilizotengenezwa na Kampuni ya Huawei yaliyofanyika katika ukumbi wa Von Naumann, Jijini Shenzhan, China.
Katika maonyesho hayo zilishuhudiwa teknolojia za kisasa ambazo ni pamoja na G5, Akili Unde, huduma za Wingu, ,miundombinu ya mawasiliano inavyotumika katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, madini, elimu, usafiri, bandari, huduma za kifedha na Miji Janja.
Waziri Kairuki alisema Tanzania itaendeleza uhusiano uliokuwepo zaidi ya miaka 10 katika miradi ya TEHAMA ikiwemo upanuzi wa Mkongo wa Taifa, ujenzi wa Miundombimu vijijini na miradi ya uwajibikaji kwa jamii.
Lengo la ushirikiano huo alisema Waziri huyo kuwa ni kuboresha utoaji wa huduma za umma kwa kutumia teknolojia za kisasa na kuimarisha uchumi wa kidijitali wa Tanzania.





Comments
Post a Comment