KAIMU WAZIRI BIASHARA AKAGUA MWENENDO WA BEI MASOKO, UNGUJA
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
KAIMU Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Sharrif Ali Sharrif, leo 25 Februari 2026 amefanya ziara katika masoko mbalimbali Unguja kukagua utekelezaji wa bei elekezi kwa bidhaa za vyakula uliotolewa na Serikali katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Katika ziara hiyo alizungumza na wafanyabiashara kupata mrejesho wa moja kwa moja kuhusu upatikanaji na bei za bidhaa muhimu
Anasema wafanyabiashara wameonyesha ushirikiano mkubwa kwa kutii agizo la serikali kwa kuzingatia bei elekezi jambo ambalo limechangia kulinda maslahi ya wananchi.



Comments
Post a Comment