LONGIDO WAASWA KULINDA IKOLOJIA HIFADHI YA JAMII ENDUIMENT


Na Sixmund Begashe, Arusha

Wananchi wa Wilaya ya Longido wamezidi kunufaika na matunda ya uhifadhi wa maeneo yaliyohifadhiwa kisheria zikiwemo Hifadhi ya Taifa Arusha na Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro (KINAPA).

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji kwenye Mkutano wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba na wananchi wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha. 


Amesema kuwa, kwa mwaka, 2024/2025, Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya Enduimet imepokea kiasi cha TShBilioni 1.3, huku Halmashauri ya Wilaya ya Longido imepokea zaidi ya TSh.Milioni 700 kupitia Utalii wa uwindaji na wa picha. 

                         

Waziri Ashatu ameendelea kuwaasa wananchi hao, kuendelea kushirikiana na Wizara hiyo ili kulinda Ikolojia ya Hifadhi hizo dhidi ya uharibifu ukiwemo uingizaji wa mifugo, uchomaji wa moto pamoja na ujangili.



Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA