CCM: TUNAAMINI KATIKA SERIKALI YA MUUNDO WA KITAIFA ZANZIBAR


                                      Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinaamini mfumo wa Serikali ya Umoja wa kiTaifa ndio mfumo bora na salama wa kiutawala, Zanzibar.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis akizungumza Mjimi Unguja 27 Februari 2026 alisema kuwa wananchi wanatarajia vyama vilivyopata kura nyingi vitasaidiana kuunda serikali kwa maslahi mapana ya nchi.

Alisema hayawezi kupuuzwa matakwa ya sehemu moja ya nchi akirejea chaguzi zilizopita ambapo takribani viti vya Uwakilishi Pemba vilichukuliwa na CUF enzi hizo na CCM kushinda vya Unguja.

"Pemba viti vyote vilikuwa CUF enzi hizo na matokeo yalikuwa kwa asilimia 51 kwa 49 na ACT kwa asilimia zao 23 za sasa huwezi kuwapuuza" alisema Mbeto.

Alibainisha kuwa kwa misingi hiyo CCM ndio maana inaendeleza utamaduni wa mazungumzo na maridhiano kwa ajili ya ustawi wa nchi na sio vyama vya siasa.

Alibainisha kuwa awamu ya pili ya Dkt. Shein mawaziri ilikuwa nusu kwa nusu chini ya muundo wa serikali ya umoja wa Kitaifa ambayo iliasisiwa na Rais mstaafu, Amani Abeid Karume ambaye kwa sasa yeye na mstaafu mwenzake Dkt. Ali Mohamed Shein wanaiwakilisha CCM katika mazungumzo ya maridhiano na ACT Wazalendo.

"Huwezi kuwapuuza ndio ukweli kuwa wananchi wanafanya maamuzi kwa kuwapa majimbo lengo kutaka ushiriki wa pamoja wa kuunda serikali" alisema Mbeto.

Mwenezi huyoo alisisitiza kuwa mazungumzo yanaendelea vizuri na maridhiano yakifikiwa yatawasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu Taifa.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA