DKT. MAGEMBE: HAKUNA MGONJWA WA KIPINDUPINDU, CHUKUENI TAHADHARI
Na Hassan Kimweri, WAF - Morogoro
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko.
Amewataka wananchi kuepuka uchafuzi wa mazingira, kuwa na matumizi sahihi ya maji safi na salama na unawaji wa mikono.
Dkt. Magembe ametoa rai hiyo Februari 25, 2026 katika tamko alilolitoa la mwenendo wa magonjwa ya mlipuko na udhibiti wa kipindipindu nchini na takriban mwezi mmoja sasa hakujatokea mgonjwa wa kipindupindu.
"Serikali imejipanga kufuatilia na kutoa huduma dhidi ya magonjwa yote ya mlipuko na itaendelea kutoa taarifa mara kwa mara iwapo kutakuwa na mabadiliko katika mwenendo wa maambukizi au endapo kutahitajika kuchukua hatua zaidi," amesema Dkt. Magembe.




Comments
Post a Comment