RAIS DKT. SAMIA, NMB WAMPONGEZA MSHINDI DÀEGU MARATHON 2026


                                            Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza waTanzania wapenda michezo kumpongeza mwanariadha, Gerald Geay kwa kuwa mshindi wa kwanza, kwa mara ya pili mfululizo, na Emmanuel Dinday kwa kuwa mshindi wa tatu katika Mbio Ndefu za Daegu (Daegu Marathon) 2026 zilizofanyika nchini Korea Kusini. 

"Mlijiandaa vizuri, mmejituma kwa bidii na mmestahili ushindi" anaandika Rais  Dkt. Samia kwenye mitandao yake ya kijamii na kuongeza kuwa mafanikio hayo yanaimarisha hadhi yenu ya kimichezo kimataifa, yanaitangaza na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Pia ni funzo na hamasa kwa wanamichezo wengine na timu zetu kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali. 

Serikali itaendelea kuweka na kuimarisha mazingira yatakayowawezesha kufanya maandalizi mazuri na kuwa washindani bora kote mnakokwenda.

NMB imesema kuwa waTanzania Wanapowania kufika mbali, sisi tunahakikisha wana pa kuanzia.

Tunajivunia kumwezesha Gabriel Geay kutwaa ubingwa wa Daegu Marathon 2026 kwa mara ya pili mfululizo.

Uthubutu wa Mtanzania hauna mipaka, NMB tunawekeza kwenye Ubora na Ubingwa wa Mtanzania. Hongera Gabriel, fahari ni yetu sote, wanasema NMB katika kurasa zao za kijamii.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA