TUME, MUFTI WATETA MATUKIO 29 OKTOBA 2025


TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Februari 27, 2026 imekutana na  Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislam (BAKWATA), Mufti Sheikh, Alhaj Abubakar Zubeir. 

Mkutano huo wa Tume na Mufti umefanyika katika Ukumbi wa Lake Tanganyika uliopo Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini hapa.


Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.

Hivi karibuni Mamlaka ya Uteuzi imeiongezea Tume muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februari, 2026 ili Tume iweze kukamilisha uchunguzi wa matukio hayo ambapo imetakiwa ikamilishe kazi na kuwasilisha Taarifa yake kabla au ifikapo tarehe 3 Aprili, 2026. 

Kwa sasa Tume inaendelea na mahojiano na watu mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA