WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA BELARUS ATUA NCHINI, ZIARA YA KIKAZI

                                      Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Belarus, Maxim Ryzhenkov, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia 28 Aprili hadi 30, 2026, kufuatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mahmoud Thabit Kombo.

Mheshimiwa Ryzhenkov amewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) na  alipokewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe, pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Belarus nchini Dzmitry Krasouski.

Katika ziara hiyo, Ryzhenkov anatarajiwa kufanya mazungumzo ya pande mbili na mwenyeji wake, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, 28 Aprili 2026, jijini Dar es Salaam pia atakutana na viongozi wengine wa Serikali kwa lengo la kuendeleza na kupanua ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Belarus pamoja na kukuza ushirikiano wa kiuchumi katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA