TANZANIA, CHINA WAINGIA MAKUBALIANO UBORESHAJI HUDUMA ZA AFYA NCHI


 Na Hassan Kimweri, WAF - Kagera 

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania na China zimefikia muafaka wa kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya kwa lengo la kuboresha huduma za tiba, tafiti, mafunzo ya wataalamu wa afya na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe amesema hayo 30 Mei 2026 ambapo makubaliano hayo yametokana na mazungumzo yaliyofanyika kati ya Waziri wa Afya, Mohammed Mchengerwa na wa China, Haichao Lei wakati wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), uliofanyika Geneva, Uswisi.

Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China tumekubaliana wataalamu wetu waandae andiko dhana na mpango wa utekelezaji kwa kuanzia na uboreshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera pamoja na utanuzi wa huduma za upasuaji wa moyo kwa watoto JKCI, makubaliano haya yatasaidia uboreshwaji wa huduma kwa wananchi," alisema Dkt. M

Alibainisha kuwa maeneo makuu ya ushirikiano ni pamoja na kuimarisha huduma za rufaa katika Hospitali ya Mkoa ya Kagera, mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko, kuboresha huduma za matibabu na upasuaji wa moyo kwa watoto pamoja na mafunzo ya watumishi wa Afya katika nyanja za tiba, tafiti na ubunifu.

Mganga mkuu  huyo wa serikali  alisema pande hizo mbili zimekubaliana kuwezesha wataalamu wa afya kutoka Tanzania kwenda China kwa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu, huku wataalamu kutoka China nao wakija nchini kubadilishana uzoefu na ujuzi.

Ameishukuru Serikali kwa kudumisha ushirikiano na mataifa mengine pamoja na Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Kagera kwa kuwezesha ziara ambayo imeibua fursa za ushirikiano huo wenye manufaa kwa maendeleo ya sekta ya afya nchini.









Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA