HOTELI DAR ZAFANYIWA TATHMINI KUELEKEA AFCON 2027


                                   Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo amekutana na timu maalum iliyoundwa na wizara hiyo iliyoanza kufanya tathmini ya ubora wa hoteli na kuzipangia madaraja ikiwa ni maandalizi ya Afcon 2027.

Akizungumza na wataalam hao walioanza kazi hiyo jijini Dar es Salaam na ambao watakwenda mikoa mbalimbali nchini kutathmini na kuzipanga hoteli katika madaraja, Dkt. Abbasi amesema zoezi hilo ni muhimu ili maeneo hayo yawe tayari kupokea wageni na kuwapa si tu huduma bali pia mandhari bora.

“Mimi nimekaa kule michezo kwa muda kidogo nawajua aina ya mashabiki wanaokuja katika Afcon. Tutarajie wanakuja nchini watu wanaopenda vitu vizuri na huduma nzuri sasa hiyo ikichangika na matokeo ya uwanjani mtu kafungwa au kashinda vyote vinamfanya akirudi hotelini ahitaji ubora wa juu wa huduma lakini mandhari yenyewe ya hoteli,” alisema Dkt. Abbasi.

Ametumia fursa hiyo kuwataka wamiliki wa hoteli hasa kwa kuanzia na mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kilimanjaro na Arusha kutoa ushirikiano katika zoezi hilo ikiwemo pia kufanyiakazi maboresho stahiki watakayopewa na wataalamu wetu wanaotumia mwongozo uliotolewa kimataifa.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA