MBETO: CCM TUMEPOTEZA KIOO CHA UPATANISHI


                                      Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kimemtaja aliyekuwa Waziri  wake wa Nchi  Ofisi ya Waziri  Mkuu Sera, Bunge na Uratibu,  William  Vangimembe Lukuvi,  amekuwa  kamusi iliosaidia kufafanua na kuelekeza kila alipohitajika kutoa ushauri katika mambo  ya msingi.

CCM kimesema kiongozi huyo alikuwa  kiungo na kiraka kilichoziba lolote  katika nyakati  zote ngumu aidha kwa masuala ya Kisiasa, kiutendaji  na Kiutawala. 

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo,  Khamis Mbeto Khamis  ameeleza hayo kwa masikitiko, huzuni na fadhaa kufuatia kifo cha mwanasiasa huyo kilichotokea Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma jana 25 Machi 2026.

Mbeto alisema Tanzania imepoteza kiongozi wake madhubuti, jasiri,  mzalendo na mshauri muhimu wa vipindi vyote  katika maisha   ya kiongozi huyo. 

Alisema  kuna mambo muhimu  sana yatakayofanya Lukuvi azidi kukumbukwa na jamii katika  utumishi wake kwa kuwa kioo kilichoakisi tija na utatuzi wa changamoto katika Siasa, Utumishi na Utawala.

"Kuwa kwake katika Utumishi kwa Muda Mrefu kumkuzia johari ya maarifa yake, uzoefu na upeo  wa kupambanua mambo  kila alipohitajika  kwa niaba ya nchi yake" alisema Mbeto 

Aidha Katibu huyo Mwenezi alisema licha ya kuwa  Mbunge pekee aliyekaa Bungeni kwa  muda mrefu zaidi   akitumikia Jimbo la Isimani Mkoani Iringa kwa miaka 30 tangu 1995 .

Mbeto alisema Lukuvi alikuwa Kiongozi jasiri,  shuupavu, mtiifu na muaminifu kwa nyakati zote.

"Lukuvi ameondoka  duniani akiwa ameshiba siha ya uaminifu na uzalendo ,  mchapakazi asiyechoka kutumikia nchi na chama chake" alibainisha mwenezo huyo.

Mbeto akiutaja  ujasiri wake, alisema alikuwa mahiri  wa kupatanisha na kusuluhisha tofauti za kimtazamo zinapochomoza ndani ya Serikali na chama na kuyaweka mambo sawa. 

"Hakuwahi kutajwa kama kiongozi shabiki au shawishi wa makundi ya hasama.  Hakuwa kiongozi aliyeingilika kirahisi au kumtoa katika reli ya msimamo wake,  kwa chama na Taifa lake" alisema Mbeto na kuongeza kuwa CCM imehuzunishwa sana na kifo chake.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA