TANZANIA, SWEDEN KUIMARISHA DIPLOMASIA, USHIRIKIANO KIMATAIFA
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngwaru Jumanne Maghembe 04 Juni 2026, ameshiriki hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Sweden iliyofanyika katika makazi ya Balozi wa Sweden jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo imeendelea kudhihirisha uhusiano wa muda mrefu wa urafiki na ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri Maghembe alieleza kuwa Tanzania na Sweden zimeendelea kufurahia uhusiano imara wa kidiplomasia unaojengwa katika misingi ya kuheshimiana, kuaminiana na kushirikiana kwa manufaa ya wananchi wa mataifa yote mawili.
Aidha, alisisitiza dhamira ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha ushirikiano huo katika maeneo ya biashara, uwekezaji, elimu, teknolojia na maendeleo endelevu.
Maadhimisho hayo yameakisi urafiki wa kudumu na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote mbili, huku yakifungua fursa zaidi za kuendeleza mahusiano ya kimkakati kati ya Tanzania na Sweden.
1.
2.










Comments
Post a Comment