KITENGO MAAFA WIZARA AFYA WAKUTANA NA WADAU MOROGORO
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
WIZARA ya Afya kupitia Kitengo cha Dharura na Maafa kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu.
Wanafanya kikao kazi chenye lengo la kupima matumizi ya rasimu ya Mwongozo wa kutuma Timu ya Wataalam kwa ajili ya kukabiliana na matukio ya dharura na maafa ndani na Nje ya Nchi (Personnel deployment Guideline for Public Health emergencies) na wadau wengine ni wara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Mambo ya Ndani, Jeshi la Polisi na Wataalam wengine.
Aidha, Juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kukabiliana na matukio ya dharura na maafa katika jamii ya watanzania zimeungwa mkono na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Amref Tanzania na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambao kupitia mradi wa Pandemic Fund wamewezesha timu ya Wataalam kufanya kikao kazi hicho.
Kikao kazi hicho kinatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku mbili tarehe 3-4 Juni,2026 Mkoani hapa huku mategemeo makubwa yakiwa ni kutoka na mwongozo utakaowezesha wataalamu kwenda kukabiliana kipindi cha matukio ya dharura mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika jamii ya Watanzania au nchi zingine.




Comments
Post a Comment