WABUNGE DRC WATEMBELEA KAMPUNI YA KUSAFISHA DHAHABU DODOMA
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
UJUMBE wa Wabunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, 14 Mei 2026, umetembelea kampuni ya Eyes of Africa Limited Mjini Dodoma inayojihusisha na usafishaji wa dhahabu, ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya mafunzo na kubadilishana uzoefu nchini Tanzania.
Katika ziara hiyo, wajumbe hao wamepata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na kampuni hiyo ikiwemo mchakato wa usafishaji wa dhahabu, viwango vya ubora pamoja na mchango wa sekta ya madini katika kukuza uchumi wa Tanzania.
Aidha, ujumbe huo ulielezwa kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika kuongeza thamani ya madini, kuvutia uwekezaji na kuimarisha biashara ya kimataifa kupitia rasilimali madini.
Wajumbe hao pia walionesha kuvutiwa na hatua zinazochukuliwa na Tanzania katika usimamizi wa sekta ya madini pamoja na juhudi za kuongeza thamani ya rasilimali za nchi kwa manufaa ya maendeleo ya kiuchumi.



Comments
Post a Comment