USHIRIKIANO KIKANDA DHIDI YA UJANGILI UNAOVUKA MIPAKA WAJADILIWA


                                     Na Mwandishi Wetu, Nairobi, Kenya 

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda katika vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori na mazao ya misitu unaovuka mipaka ya nchi.


_Rais wa Baraza la 14 la Uongozi wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Lusaka (14th Bureau of Governing Council) ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akifungua kikao cha Baraza hilo jijini Nairobi, Kenya._

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Baraza la 14 la Uongozi wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Lusaka (14th Bureau of Governing Council) ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akifungua kikao cha Baraza hilo jijini Nairobi, Kenya.

Dkt. Kijaji amesema ushirikiano wa kikanda ni silaha muhimu katika kupambana na mitandao ya kimataifa inayojihusisha na biashara haramu ya wanyamapori, ujangili na mazao ya misitu.

Ameongeza kuwa dhamira ya Tanzania katika kuimarisha uhifadhi wa maliasili imeendelea kuonekana kupitia hatua mbalimbali za kitaifa zilizotekelezwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Alisema tangu nchi hiyo ichukue uongozi wa Baraza hilo jijini Arusha. Aidha, amesisitiza kuwa Tanzania imewekeza katika uhifadhi shirikishi unaozihusisha jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi.

Vilevile, Dkt. Kijaji amesisitiza kuwa rasilimali za wanyamapori na misitu  si mali ya taifa moja pekee, bali ni urithi muhimu wa Dunia unaopaswa kulindwa kwa nguvu zote kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.s

Aidha, ameongeza kuwa juhudi hizo zinaonyesha wazi kuwa mafanikio katika uhifadhi Wanyamapori na misitu hayawezi kupatikana kwa matamko ya kisiasa pekee, bali yanahitaji utekelezaji wa vitendo, ubunifu, uwekezaji na hatua zinazoleta matokeo yanayoonekana.

Kikao hicho kilichoongozwa na Dkt. Kijaji kimewakutanisha nchi wanachama wa Mkataba wa Lusaka, zikiwemo Kenya, Tanzania, Congo Brazzaville, Zambia na Liberia.

Aidha, kikao hicho kimetokana na maazimio yaliyofikiwa katika Kikao cha 14 cha Baraza la Usimamizi wa Mkataba wa Lusaka kilichofanyika mwezi Mei 2025 jijini Arusha, Tanzania.

Sambamba na hayo, Dkt. Kijaji alipata fursa ya kuzindua Mpango Mkakati wa Sekretarieti ya Mkataba wa Lusaka wa mwaka 2025–2030 unaolenga kuimarisha mapambano dhidi ya makosa ya wanyamapori na mazao ya misitu yanayovuka mipaka ya nchi.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA