TANZANIA, ZAMBIA ZAJADILI KUKUZA BIASHARA


                                      Na Mwandishi Wetu, Tunduma

NAIBU Waziri wa Fedha, Mhandisi Mshamu Ali Munde, ameshiriki Mkutano wa Tano wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (5th Joint Trade Committee - JTC) kati ya Tanzania na Zambia, uliofanyika Mjini Tunduma, Mpakani mwa Tanzania na Zambia, katika Mkoa wa Songwe.

Pamoja na mambo mengine wamejadili kwa kina namna ya kukuza biashara kwa faida ya nchi hizo mbili.

Katika mkutano huo pande zote mbili zilijadili kuhusu namna ya kuboresha mazingira ya biashara na miundombinu yake ikiwemo sekta ya usafirishaji. 

Sekta hiyo inatajwa kuwa itakayochochea ufanyaji biashara na kutoa fursa zaidi kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania na Zambia.

Mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha ngazi ya wataalamu na kufuatiwa na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Fedha, Uchukuzi, Viwanda na Biashara Pamoja na Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zambia.

Viongozi wengine wa Serikali ya Tanzania walioshiriki Mkutano huo ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Millya, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Denis Londo pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Serikali ya Zambia.



Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA