TANZANIA, SERBIA KUIMARISHA USHIRIKIANO KISEKTA, DIPLOMASIA


                                    Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAIMU Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ellen Maduhu, 18 Mei 2026 amekutana na kuzungumza na Balozi Mkazi wa Jamhuri ya Serbia nchini, Jovica Topalović, katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Serbia.

Katika mazungumzo hayo, Balozi Topalović amewasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Serbia, Aleksandar Vučić, kwenda kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Vilevile, pande hizo mbili zimejadili dhamira ya pamoja ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati, ikiwemo biashara, uwekezaji, utalii, kilimo, afya, elimu pamoja na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).



Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA