RAIS RUTO; E.A.C TUNA MAADUI WATATU
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto amebainisha kuwa nchi za Afrika Mashariki, zinakabiliwa na maadui watatu ambao inabidi kupambana nao ili kujiletea maendeleo.
Akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 05 Mei 2026 kwa mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa Rais wa Kenya, aliwataja adui hao ni umaskini, ukosefu wa ajira kwa vijana na maendeleo.
Alisema Rais Ruto kuwa maadui wa Tanzania sio Wakenya na maadui wa Kenya sio Watanzania, j zetu ni ukosefu wa kazi, umaskini na ukosefu wa maendeleo. Hivyo tujitahidi kupambana na maadui hawa ili kujiletea maendeleo na kuongeza ajira kwa vijana.
"Ushirikiano wetu si chaguo bali ni wajibu wa kihistoria kwa ustawi wa watu wa pande zote mbili" alisema Rais Ruto kutaka kuimarishwa kwa umoja, ushirikiano wa kikanda, biashara na maendeleo ya pamoja kati ya nchi za Afrika Mashariki.
Alieleza kuwa Kenya na Tanzania zina nafasi muhimu katika kukuza uchumi wa eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akihimiza kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa haya mawili na kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana na umaskini ili kujiletea maendeleo endelevu yenye manufaa ya watanzania na wakenya.
Rais Ruto alisema kuwa hatua ya pamoja ya kuwekeza katika miradi mikubwa ni muhimu kwa nchi za Afrika Mashariki ili kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya ukanda na kuongeza kuwa Afrika Mashariki ina rasilimali za kutosha, lakini kinachohitajika ni maamuzi ya pamoja na uwekezaji wa kimkakati ili kuzitumia kikamilifu rasilimali hizo.
Alisema Uwekezaji katika mradi huo wa Tanga gharama zake ni kubwa ambao unafikia mabilioni ya dola na kubainisha kuwa Kenya imeamua kuunga mkono ujenzi wa kiwanda hicho nchini Tanzania kama ishara ya mshikamano wa kikanda.
Rais Ruto alieleza kuwa uchaguzi wa kuamua kuiunga mkono Tanga unatokana na uwepo wa miundombinu muhimu kama Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), ambalo litarahisisha usafirishaji na usambazaji wa mafuta na alisisitiza kuwa huo ni mwanzo wa safari mpya ya Afrika Mashariki kuelekea kujitegemea, umoja na ustawi wa pamoja.
"Kupitia mradi huo, mapato yatabaki ndani ya nchi za Afrika Mashariki, hali itakayosaidia kukuza uchumi wa ndani pamoja na kuongeza ajira kwa maelfu ya vijana" alisisitiza.
Rais Ruto pia alizungumzia uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya Tanzania na Kenya, akibainisha kuwa mataifa hayo mawili yameunganishwa na historia, utamaduni na mahusiano ya muda mrefu ya kijamii na kiuchumi na alitoa wito wa kuendeleza urafiki huo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Hotuba hiyo imeelezwa kuwa ya kihistoria, ikitoa dira ya ushirikiano mpana zaidi katika nyanja za nishati, biashara na miundombinu, huku ikisisitiza mshikamano kama nguzo kuu ya maendeleo ya ukanda wa Afrika Mashariki.







Comments
Post a Comment