RAIS DKT. MWINYI ASHIRIKI SALA YA JENEZA YA MAREHEMU KOCHA ABDULGHAN MSOMA


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika sala ya jeneza ya Kocha wa zamani wa Malindi, Small Simba na Zanzibar Heroes, marehemu Abdulghani Himid Msoma, aliyefariki 23 Mei 2026, wakati anapatiwa matibabu nchini India.

Sala hiyo ilisaliwa katika Msikiti wa Jamiu Zinjibar, Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Wakati wa uhai wake, marehemu Msoma aliwahi pia kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),, ikiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Viwanja vya Ndege Zanzibar.

Kocha huyo ambaye alizifanya Malindi na Small Simba kuleta upinzani mkubwa kwenye Ligi ya Muungano miaka  ya 1980/1990 na kuzisumbua Simba, Yanga, Pamba, Majimaji na zingine.

Aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF) kabla afya haijaanza kumtatiza, amezikwa leo 25 Mei katika Makaburi ya Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA