RAIS DKT. MWINYI ASHIRIKI DUA, ATOA POLE
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika dua maalum ya kumuombea marehemu Sheikh Abuubakar bin Said Al-Abassy.
Dua hiyo imesomwa jana 02 Mei 2026, katika Ukumbi wa Majid uliopo Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Dkt. Mwinyi amemuelezea mwanazuoni huyo kuwa alikuwa mtu mwema, mwenye upendo na aliyewafundisha watu wengi elimu ya dini.
Wakati huo huo, Rais Dkt. Mwinyi ametoa mkono wa pole kwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mhe. Nadir Abdullatif Al-Wardi, pamoja na familia yake kufuatia kifo cha baba yao mzazi aliyefariki nchini India.
Rais Dkt. Mwinyi alifika nyumbani kwa familia hiyo, Chukwani Buyu, kutoa mkono wa pole na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki cha msiba mzito.
_Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akisalimiana na Sheikh Said, mtoto wa marehemu Sheikh Abuubakar bin Said Al-Abassy, alipowasili kushiriki dua maalum ya kumuombea marehemu huyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Majid, Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, jana 2 Mei 2026._






Comments
Post a Comment