RAIS DKT. MWINYI AKUTANA NA WAKUFUNZI, WANAFUNZI NDC-TZ, IKULU ZANZIBAR

                                          Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na ujumbe wa wakufunzi waandamizi elekezi pamoja na wanafunzi 72 wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC-TZ) kutoka mataifa mbalimbali 17, waTanzania wakiwemo, pamoja na watumishi waandamizi wa Serikali.

Ujumbe huo uliongozwa na Balozi Meja Jenerali Wilbert Augustin Ibuge, ambaye ni Mkuu wa Chuo hicho, walipofika Ikulu Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo leo 06 Mei, 2026.

                            

_Ujumbe wa wakufunzi waandamizi elekezi pamoja na wanafunzi 72 wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC-TZ) kutoka mataifa 17 mbalimbali, ikiwemo Tanzania, pamoja na watumishi waandamizi wa Serikali, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, walipomtembelea Ikulu, Zanzibar leo.                                                                                                                                               

_Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na _Ujumbe wa wakufunzi waandamizi elekezi pamoja na wanafunzi 72 wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC-TZ) kutoka mataifa 17 mbalimbali, walipomtembelea Ikulu, Zanzibar 

_Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akipokea zawadi yenye mchoro unaoashiria ushirikiano kati ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC-TZ) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho, Balozi Meja Jenerali Wilbert Augustin Ibuge, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu, Zanzibar 06 Mei, 2026._

   

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA