PROF. SHEMDOE ATAKA USAFI UWE AJENDA KUU SERIKALI ZA MITAA
Na OWM - TAMISEMI, Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewataka washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Afua ya Uthibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Miji, kuhakikisha suala usafi wa mazingira linakuwa ajenda ya kudumu katika vikao vyote vitakavyofanyika katika ngazi zote za Mamlaka za Serikali za Mitaa. Hatua hiyo ichukuliwe ili kuwezesha miji na majiji nchini kuwa katika hali ya usafi.
Ameainisha kuwa, usafi wa mazingira ukizingatiwa katika ngazi zote za Mamlaka ya Serikali za Mitaa utapunguza milipuko ya magonjwa na matumizi ya fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawa.
Usafi ukifanyika fedha zitakazookolewa zitaelekezwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hivyo amewataka maafisa hao kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kupunguza milipuko ya magonjwa na matumizi ya ununuzi wa dawa.

.jpg)



Comments
Post a Comment