MBETO: NI MAKOSA KUDHANI DEMOKRASIA MAANA YAKE HADI CCM ING'OKE MADARAKANI


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema ikiwa tafsiri na maana   ya demokrasia kwa upinzani ni kuona  CCM  ikishindwa Uchaguzi, kupoteza Viti vya Udiwani, Ubunge na Uwakilishi, hiyo si tafsiri wala  mantiki sahihi ya neno demokrasia.

Aidha CCM kimeapa  hakiwezi kushindwa na  vyama vilivyoundwa kuanzia Mwaka 1992, kwa kudhani  tayari viwe na nguvu  za  kukishinda chama kilichoshika  madaraka miaka zaidi ya 60.

Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati  Maalum ya NEC  Zanzibar, Idara ya Itikadi,  Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto  Khamis , alipozumgumza na wanahabari, ofisini kwake CCM Kisiwandui  Unguja. 

Mbeto alisema  nguvu za chama chochote cha siasa duniani,  ni  umri na uimara wa chama hicho raslimaliwatu na fedha, mitaji na vitega uchumi,  sera makini,   oganaizesheni  ilioshamiri na mtandao madhubuti wa kisiasa.

Alisema CCM  ni chama kilichojijenga kimtandao kipo kila kona Tanzania, kina rasilimali watu, mitaji na vitega uchumi,  ivyo si jambo rahisi kudondoshwa  na  vyama vilivyoundwa mwaka 1992.

"Ni ajabu kusikia upinzani ukidai kura zake zinaibiwa. Vyama hivyo bado vichanga kisiasa  havina ubavu wa kushindana na CCM.  Hata timu changa za soka hazihimili  mikiki mikiki dhidi ya Simba au Yanga Uwanjani" alisema Mbeto. 

Aidha  akisema bila kukitaja jina  chama chochote  cha upinzani, alidai kimeweza kununua jengo jipya la Ofisi  zake baada ya  kulipwa ruzuku  kutoka katika Serikali  za CCM huku chama hicho kikijigamba  kina uwezo wa   kuidondosha CCM.

Alipoulizwa iwapo Serikali za CCM  zipo tayari kufanya  mabadiliko ya katiba, mifumo ya uchaguzi, kitaasisi na  sheria ya  Uchaguzi, Mbeto alijibu kuwa kipo tayari ingawaje kusitokane na  shindikizo au kwa vitisho 

"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi  kabla hajaondoka madarakani mwaka 2030  Tanzania itapata Katiba mpya. Lakini hata ikipatikana Katiba  , mabadaliko ya mifumo na sheria, upinzani  haujapata na havina uwezo wa kuishinda CCM" alieleza.

Katibu  huyo Mwenezi  alisema ikiwa neno demokrasia  kwa tafsiri  ya upinzani hadi  pale kishindwe uchaguzi, vyama hivyo vitasubiri  kwa miaka mingi kwa kuwa CCM bado kitaendelea kuungwa mkono wananchi na kuongoza dola. 

"Nimemsikia Mwenyekiti  wa ACT  Wazalendo  Othman Masuoud Othmam akidai CCM kimejiweka madarakani. Muulizeni kimejiweka kivipi? Uchaguzi haukuafanyika. Vyama havikushriki Uchaguzi na je, Tume ya Uchaguzi haikumtangaza mshindi ? " Alihoji  Mwenezi huyo.

Mbeto alimtaja  Mgombea  huyo wa  Urais  Zanzibar  kupitia  ACT Wazalendo, hajawa na  sifa za kumshinda Mgombea Urais wa CCM Rais  Dkt. Hussein  Ali Mwinyi na cha ajabu amekuwa akisimama na kudai ameibiwa kura.

"Ni kura zipi  hizo alizoibiwa Othman. Yeye alikuwa wapi  wakati kura zikiibiwa .Ziko wapi  na kwanini hakuwakamata walioiba. Kama kuiba Kura  jambo  rahisi yeye  na chama chake walishindwaje kuiba? " alishangaa Mbeto.

Hata hivyo Mwenezi  huyo alisema kwa nafasi ya Urais  Zanzibar, alimtaja  Othman kuwa. Mwanasiasa mpya  asiye na   umaarufu ndani na nje ya ACT  ,  kwa asili na historia ya Siasa  za Zanzibar,  si mtu anayetambulika na kukubalika.


 

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA