MBETO: NI KITUKO KUDAI TANZANIA HAINA DEMOKRASIA, UHURU WA KUABUDU  


                                          Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kwa namna yoyote kuihusisha Tanzania na ubaguzi wa aina yoyote au kudai inakiuka msingi ya demokrasia huku ikikandamiza uhuru wa kuabudu ni kituko kipya kuwahi kutokea.

Aidha chama hicho kimesisitiza kuwa yeyote anayetoa madai hayo , haijui historia ya kweli ya Tanzania  mbele ya uso wa dunia wala halisi iliyopo nchini tangia uhuru.

Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum  ya NEC  Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis aliyesema wanaodhani watamudu kuipaka matope Tanzania, wajitafakari zaidi. 

Mbeto alisema kama kuna Mataifa Duniani ambayo tokea yapate Uhuru wake yamekuwa yakiongozwa kwa kuheshimu utawala wa sheria, kuenzi  utu, haki za binadamu na demokrasia, Tanzania ni miongoni mwa Mataifa hayo.

Alisema kimsingi  na ukweli  usiopingika kwamba  Tanzania si mshrika wa mapenzi ya jinsia moja, haishabikii ushoga na ubasha pia haliwezi kuwa Taifa kibaraka lisilo na msimamo imara. 

"Tunaelewa kuwa ukitaka mbwa wako afe haraka mpe jina baya. Jaribio lolote la kutaka kuipaka matope Tanzania kwa namna yoyote ya kisingizio  cha uvunjaji wa haki  za binadamu  na demokrasia, madai hayo hayana ushahidi wala mashiko"  Mbeto. 

Alieleza kuwa hatua ya chama kimoja cha siasa   kususia Uchaguzi  mkuu kwa sababu zao binafsi, kutaka kukinukisha na kukiwasha , hakuhalalishi kuthibitisha  madai ya kukosekana utawala bora, demokrasia au kufinya uhuru wa watu kuabudu. 

"Tanzania ni Mwalimu Mkuu wa kufundisha  maana ya demokrasia, utawala bora na kuenzi haki za binadamu Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kama wapo wanaopaza sauti zao kwa shinikizo, mihemko na unazi, waache kufanya hivyo" alisema Mbeto.

Pia Katibu huyo Mwenezi  aliongeza kusema hakuna chama cha siasa kilichozuiwa kisishiriki Uchaguzi Mkuu 2025 au kukamatwa kwa baadhi ya wanasiasa na kuwaweka ndani kimaonevu bila uvunjaji wa sheria  za nchi.

"Tanzania si koloni la Taifa lolote Duniani. Limepata auhuru wake baada ya mapambano ya kisiasa yenye hoja na kuanza kujitawala. Tabia ya vitisho, ubabe na mikwala zikome toka sasa" alisisitiza.

Mbeto alisema iwapo kama kuna baadhi ya Mataifa yalitegemea kuutumia mwanya wa Uchaguzi Mkuu ili Tanzania izame katika ghasia  ambazo hatimae zingefanikisha Mapinduzi na  kuondoa utawala halali uliowekwa na wananchi, wakajipange upya.

"Hatuwezi kuishi kwa kupimana mbavu kila uchao. Waafrika wameshakataa aina yoyote  ya utumwa tokea enzi ya Ukoloni ukiwemo utumwa wa kudumazwa akili, maarifa na kushindwa kutoa maamuzi" Mbeto alisema kwa kujiamini.

Kadhalika akitoa mifano hai, Mwenezi huyo alisema Tanzania ndio Taifa pekee  duniani lenye raia  ambao  wanaishi bila  kubaguana kwa rangi, dini na kabila badala yake  watu wake huheshimiana na kuishi kwa upendo.

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA