KAMATI ZA BUNGE JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA, DRC ZAKUTANA
Pia walifanya mazungumzo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu.
Viongozi hao wamekutana kuzungumzia namna wanavyoweza kuimarisha na kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na DRC katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, uvuvi, kilimo na mifugo.
Sekta zingine zilizojadiliwa ni miundombinu ya usafirishaji inayowezesha mwingiliano kati ya mataifa yote mawili.
Buhuni aliambatana pia na Balozi wa Tanzania nchini DRC, Said Mshana na Balozi wa DRC nchini Tanzania, Jean Pierre Massala.





Comments
Post a Comment