FIDIA, TATHMINI MAZINGIRA VYACHELEWESHA UJENZI BARABARA CHAKE-MKOANI


                                    Na Mwandishi Wetu, Pemba

MWENYEKITI wa CCM, Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba kuwa Serikali inaendelea na juhudi kuhakikisha ujenzi wa Barabara ya Chake Chake hadi Mkoani unakamilika.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, 13 Mei 2026, alipozungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Pemba katika mkutano wa kutoa shukrani baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ulioambatana na ufunguzi wa Jengo la CCM Ng’ombeni pamoja na Ukumbi wa Mikutano wa Hijaz Complex, hafla iliyofanyika Ng’ombeni, Mkoa wa Kusini Pemba.

_Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akizungumza wakati wa  hafla  hiyo.

Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM, Zanzibar, amefahamisha kuwa mradi huo umechelewa kuanza kufuatia kufanyika kwa tathmini ya kimazingira ya kutokukatwa kwa miti pamoja na utaratibu wa ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha ujenzi wa barabara hiyo.

Alibainisha kuwa Serikali inaendelea na mazungumzo ya kina ili kukamilisha mradi huo aliouelezea kuwa ni muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Kusini Pemba na nchi kwa ujumla, huku akiwataka wananchi kuwa wastahamilivu.


_Baadhi ya wanaCCM wakiwa kwenye hafla hiyo._

Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM, Dkt. Mwinyi amesema Chama Cha Mapinduzi kimetekeleza kwa mafanikio makubwa ahadi zake kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba kupitia ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo skuli za ghorofa, hospitali, vituo vya afya pamoja na uimarishaji wa miundombinu ya bandari kwa lengo la kuboresha huduma za kijamii na kukuza uchumi wa wananchi.

_Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar, Idara Itikadi Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis akiwa na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Kusini Pemba, Yussuf Ali Juma._

Aidha, amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa Kiwanja _Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akikata utepe kufungua Jengo la CCM Ng’ombeni._ Ndege cha Pemba ambacho kitasaidia kukifungua Kisiwa hicho kiuchumi kwa kuongeza fursa za biashara, uwekezaji na utalii, sambamba na kurahisisha huduma za usafiri kwa wananchi na wageni wanaofika Kisiwani humo.

Dkt. Mwinyi, akizungumzia suala la uimarishaji wa Chama Cha Mapinduzi, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha mambo manne muhimu ndani ya Chama, ikiwemo maadili ya wanachama, uhai wa Chama, suala la uchumi ndani ya Chama, pamoja na kusisitiza kuanzishwa kwa miradi mbalimbali mikubwa yenye tija katika maeneo yanayomilikiwa na CCM ili iwe na uchumi imara na kujiendesha kwa ufanisi.

ZZ

_Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi, akikabidhiwa zawadi yenye mchoro wa picha ya Jengo la CCM Ng’ombeni kutoka kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Kusini Pemba, Yussuf Ali Juma, baada ya mazungumzo na viongozi pamoja na wanachama katika mkutano wa kutoa shukrani baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
_

Aidha, ameeleza umuhimu wa kufufuliwa kwa madarasa ya itikadi katika kila ngazi ya Chama yatakayosaidia wanachama kufahamu wajibu wao katika kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.

Akihitimisha hotuba yake, Dkt. Mwinyi amewahakikishia wananchi na wanachama wa CCM kuwa majadiliano ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa pamoja na Chama cha ACT-Wazalendo yanaendelea vizuri, na kwamba Chama Cha Mapinduzi kinafanya majadiliano hayo kwa hekima kubwa kwa kuzingatia maslahi ya Taifa na Chama hicho.

_Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akikata utepe kufungua Jengo la CCM Ng’ombeni._

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, yupo Kisiwani Pemba kuendelea na ziara yake ya kutoa shukrani kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.


_Ukumbi wa mikutano wa Hijjaz Complex._


Comments