DKT. MWINYI: AZUNGUMZA, AWASHUKURU WAZEE CCM KISIWANDUI, IKULU ZANZIBAR
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ya maendeleo kwa lengo la kuijenga nchi na kuandaa maisha bora kwa wananchi.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, 16 Mei 2026, alipokutana na Baraza la Wazee wa Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar katika mkutano maalum wa kutoa shukrani baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2026, hafla iliyofanyika Ikulu, Zanzibar.
_Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na Baraza la Wazee wa Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Zanzibar katika mkutano maalum wa kutoa shukrani baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2026 Ikulu, leo tarehe 16 Mei, 2026._
Makamu Mwenyekiti, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa kazi muhimu iliyobakia ni kuyatekeleza kwa vitendo mambo yote yaliyoainishwa katika Ilani ya CCM ili yawe yamekamilika ifikapo mwaka 2030.
_Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi, akikabidhiwa zawadi ya kasha na viongozi wa Baraza la Wazee wa Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Zanzibar mara baada ya mkutano huo.._
Akizungumzia miradi inayoendelea ya ujenzi, amesema nia ya Serikali ni kujenga nyumba za kisasa kwa ajili ya makaazi ya wananchi na kuwaondoa katika majengo chakavu yaliyotumika kwa zaidi ya miaka 60 ambayo hayana usalama tena.
_Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama pamoja na Baraza la Wazee wa Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu, Zanzibar._
Aidha, ameeleza dhamira ya Serikali ya kuendelea na miradi zaidi katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii ikiwemo sekta ya afya, elimu, miundombinu, mawasiliano, bandari, barabara, viwanja vya ndege pamoja na nyumba za maendeleo za kisasa.
_Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Baraza la Wazee wa Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu, Zanzibar._
Akizungumzia suala la Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Makamu Mwenyekiti, Dkt. Mwinyi, amesema majadiliano na Chama cha ACT-Wazalendo yanaendelea vizuri na kwamba Chama Cha Mapinduzi kinazingatia maslahi ya chama hicho pamoja na Taifa kwa ujumla. Amebainisha kuwa lengo kuu ni kuwa na nchi tulivu yenye amani, umoja na kuondoa chuki miongoni mwa wananchi.
Akiwasilisha salamu za wazee, Mjumbe wa Baraza la Wazee wa CCM Zanzibar, Ndg. Waziri Mbwana Ali, amesema Baraza hilo limempongeza Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Dkt. Mwinyi, kwa kuimarisha umoja na utulivu wa nchi pamoja na kuleta maendeleo makubwa na dhamira ya kimkakati ya kuifungua Pemba.





Comments
Post a Comment