CCM YATAKIWA KUWA NA MIRADI MIKUBWA YA KIUCHUMI
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema wakati umefika kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa na miradi mikubwa ya kiuchumi kwa kutumia rasilimali zake zilizopo katika maeneo mbalimbali ili kukiimarisha kiuchumi na kuongeza uwezo wake wa kuwatumikia wanachama na wananchi.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, 10 Mei 2026, alipozungumza na viongozi na wanachama wa CCM wa Mkoa wa Kusini Unguja katika mkutano maalum wa kutoa shukrani baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohammed Shein, Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais Dkt. Mwinyi pia, amewasisitiza viongozi na wanachama kutumia maeneo yanayomilikiwa na CCM kuwekeza miradi mikubwa itakayosaidia kuongeza mapato, kuimarisha shughuli za chama na kuboresha maslahi ya watendaji wake.)
Akizungumzia maadili ndani ya chama, Dkt. Mwinyi ametoa rai ya kufufuliwa kwa Kamati za Maadili katika ngazi mbalimbali pamoja na kusisitiza matumizi ya vikao vya kikatiba katika kujadili na kuimarisha nidhamu kwa wanachama.






Comments
Post a Comment